NA JOSEA SINKALA, MBEYA.
Katika kutatua changamoto kadhaa zinazoikabili shule ya sekondari Juhudi Usongwe mji mdogo wa Mbalizi wilayani Mbeya, Mbunge wa Mbeya vijijini Mhe. Oran Njeza ameahidi kutoa fedha zaidi ya shilingi million tatu ili kuhakikisha shule hiyo inaendelea kuwa na mazingira bora.
Mbunge Njeza ametoa ahadi hiyo alipokuwa mgeni rasmi kwenye mahafali ya kwanza ya kuwaaga na kuwatunuku vyeti wahitimu 248 wa shule hiyo.
Mbunge huyo amepanga kutoa fedha shilingi million tatu laki moja na hamsini na mbili elfu ili kusaidia miundombinu mbalimbali shuleni hapo
Mhe. Mbunge ameahidi shilingi million mbili kwa ajili ya tenki la maji, shilingi laki tano kwa ajili ya walimu, vijana wa scout Tsh. 222,000 na kuunga mkono mpango wa chakula shuleni kwa kuchangia shilingi laki mbili huku akitoa motisha kwa wanafunzi waliofanya vizuri ambao amewakabidhi shilingi laki mbili na thelathini.
Ameiomba Halmashauri ya Mbeya kuendelea kuwa karibu na shule hiyo ikiwemo kutupia jicho mpango wa kujenga uzio ili kuzuia utoro na kuimarisha ulinzi shuleni hapo.
0 Comments