Header Ads Widget

MBUNGE MBEYA VIJIJINI KUPAMBANA NA KERO ZA MBALIZI SEKONDARI.

 

NA JOSEA SINKALA, MBEYA.

Mbunge wa Mbeya vijijini Mhe. Oran Njeza ameahidi kumaliza changamoto zinazoikabili shule ya sekondari Mbalizi ikiwemo ukosefu wa huduma ya maji safi shuleni hapo.

Kero kubwa zinazoikabili shule hiyo ni ukosefu huduma ya maji shuleni hapo, upungufu wa computer na uchakavu.


Akizungumza kwenye mahafali ya kuwaaga wahitimu wa kidato cha nne mwaka 2024 katika shule hiyo, Mhe. Mbunge wa jimbo la Mbeya vijijini Oran Manasse Njeza, amesema atashirikiana na kushauriana na uongozi wa jumuiya ya wazazi wa Chama cha Mapinduzi kuona namna ya kuboresha miundombinu ya shule hiyo.

Kuhusu kadhia ya maji, Mbunge Njeza amesema anakwenda kulivalia njuga suala hilo ili kuhakikisha ndani ya muda mfupi maji yanapatikana kwakuwa ni jambo la ajabu shule hiyo kutokuwa na huduma hiyo muhimu wakati mamlaka ya mji mdogo wa Mbalizi hakuna shida ya maji.

Kuhusu upungufu wa komputa, ameahidi kutoa komputa kumi ili kuhakikisha somo la TEHAMA linafundishwa kwa vitendo.

Pamoja na hayo ameipongeza shule hiyo kwa kuendelea kufundisha watoto kwa weledi na kuwa miongoni mwa shule bora katika shule za sekondari mkoani Mbeya.


Mkuu wa shule ya sekondari Mbalizi Mwal. Shija, amesema shule yake inaendelea kufanya vizuri kitaaluma kila uchao na kuboresha mazingira ya utolewaji elimu shuleni hapo na kumwomba Mbunge wa Mbeya vijijini, Chama cha Mapinduzi na Serikali kuwaunga mkono kuhakikisha baadhi ya kero zinazowakabili zinatatuliwa ili kuendelea kuwa shule ya mfano katika elimu, michezo, nidhamu na nyanja nyinginezo.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI