Header Ads Widget

MAHAKAMA YAMPA DHAMANA KADA WA CHADEMA BONIFACE JACOBO



Na, Matukio Daima App,


Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imetupilia mbali pingamizi la kuzuia dhamana kwa Boniface Jacob 'Boni Yai' kwa kueleza kuwa kiapo cha RCO wa Mkoa wa Polisi Kinondoni, Davis Msangi hayana maelezo yazida yenye kutosha kuzuia dhamana hiyo.


Sababu zilizotolewa hazina maelezo ya ziada ya kwanini mahakama isitoe dhamana. Iwapo mjibu maombi ametoa maelezo juu ya usalama wake nilitegemea muombaji (Jamhuri) ataleta uthibitisho juu ya maelezo ya mjibu maombi.


Pamoja na kwamba upande wa mjibu maombi haujaleta kiapo kinzani lakini kiapo cha muombaji haitoshi mahakama kumnyima dhamana mtuhumiwa ukizingatia hii ni haki ya kikatiba.

Mahakama hii haikubali maombi ya Jamhuri hivyo basi mjibu maombi atapewa dhamana kwa mujibu wa masharti yatakayowekwa na mahakama hii.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI