Header Ads Widget

MADIWANI MTAMA WALIA NA UBOVU WA MIUNDOMBINU YA BARABARA

 


NA MATUKIO DAIMA APP, LINDI 

Madiwani wa Halmasahuri ya Mtama wameiomba wakala wa barabara za Mijini na Vijijini TARURA kuharakisha mchakato wa ujenzi wa miundombinu ya Barabara Katika Maeneo yao.


Madiwani hao wameyasema hayo leo tarehe 22 katika kikao cha Madiwani cha robo ya kwanza wakati wa kuwasilisha tarifa za kata za halmashauri hiyo .


Diwani Kata ya Mnolela Omary Liveta amesema Halmashauri hiyo ina changamoto sana katika miundo mbinu ya barabara kila siku wanapewa taarifa ya kuanza miradi lakini haitekelezeki.  


"Changamoto ya barabara kwenye Halmashauri yetu tunapewa matangazo lakini hatujui ni lini utaanza tunawaita wananchi tunawapa taarifa lakini hatujui ni lini utaanza wananchi wanatuona sio wa kweli. amesema Liveta.


Kwaupande wake diwani wa Nyangao Mohammed Babu ameomba kujengwa kwa barabara ya Nyangao kwenda Namupa kwasababu haipitiki hata namna ya kutoa mazao ikiwemo korosho kupeleka ghalani ni changamoto.


 "Barabara ya Nyangao kwenda Namupa haipitiki hata kwa Trekta na kule kuna upimaji wa korosho hatu jui hata zitatokaje huko ziliko"alisema Babu.


Kaimu meneja Wakala wa baraara za mijini na vijijini(Tarura)Baraka Ojisa alisema baadhi ya barabara alishaoneshwa mkandarasi na wakati wowote kazi itaanza.


"Barabara Mnolela hadi Simana nikweli tulimuonesha makandarasi eneo la kazi utaratibu kuna siku 14 zakujiandaa baada ya kukabidhiwa kazi wiki hii ni ya pili wiki ijayo tunaamini kazi itaanza"amesema Baraka.


Baraka liongeza kwakusema barabara ya Namupa hadi Mihima mradi huu umebakia kutanganzwa ila wiki ijayo tutaangalia nana gani tunaweza kufanya ili barabara iyanze kupitika.


Naye mwenyekiti wa Halmashauri ya Mtama Abdallah Tipu amewataka madiwani waende waka simamie mambo ya maendeleo na waende wakafanye vikao.


"Madiwani tuendelee kufanya vikao kwenye kata zetu twendeni tukafanye kazi.Wakuu wa idara tunapoona miradi haikamiliki sisi kwetu ndiyo fimbo ya wananchi kutupigia kwahiyo tunaomba mambo yaende kama miradi ya maji basi itekelezwe kwa wakati".alisema Tipu.





Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI