Na Hamida Ramadhan Matukio Daima App Dodoma
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Ridhiwani Kikwete amesema kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru 2024, Rais Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuhitimisha sambamba na Kumbukumbu ya Miaka 25 ya kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere itakayofanyika Kanisa Katoliki la Nyakahoja Mkoani Mwanza.
Akiongea na waandishi wa habari Oktoba 9,2024 amesema kuelekea katika kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Vijana Kitaifa yanayotarajiwa kufanyika Mkoani Mwanza,
Amesema maadhimisho hayo yameanza Oktoba 8, 2024,ambapo katika wiki hiyo shughuli mbalimbali zitakazo fanyika ikiwamo kongamano la fursa na kuwajengea uelewa vijana katika masuala mbalimbali ambapo
Kikwete, ametaja shughuli zitakazofanyika kwenye wiki hiyo kuwa ni pamoja na Kongamano la kuwajengea uelewa wa fursa za ujasiriamali, ubunifu wa kidijitali katika kujifunza na kujiajiri sambamba na elimu ya Sera mpya ya maendeleo ya vijana (2007), Toleo la Mwaka 2024.
Kadhalika amesema kutakuwa na maandamano ya amani ya vijana na watashiriki 1000 wakiwa wamebeba jumbe mbalimbali ambazo serikali itazifanyia kazi.
“Kutakuwa na Maonesho ambayo hutoa fursa kwa vijana kuonesha bunifu zao na kwa wadau wa maendeleo ya vijana kutoa huduma, elimu na taarifa kwa jamii hususan zile zinazoendana na malengo ya Taasisi zao na zenye lengo la kuleta mabadiliko chanya na kuhamasisha ustawi na maendeleo ya vijana nchini,”amesema.
Kikwete ameelezea malengo ya wiki hiyo kuwa ni kuwakutanisha vijana kujadili fursa na changamoto zinazowakabili, kuhamasisha kushiriki katika program mbalimbali za usaidizi wa jamii kwa njia ya kujitolea, kuwawezesha vijana kupata uzoefu wa namna ya utekelezaji wa masuala ya kiuchumi na kijamii.
“Pia wiki hii inalenga kuwahamasisha vijana watambue kuwa wao ni sehemu ya jamii na wenye jukumu katika kushughulikia changamoto za kijamii kama vile VVU na UKIMWI, Ukiukwaji wa haki za binadamu na watoto, kushiriki katika majukumu ya kiraia ikiwamo kupiga kura na kushiriki vikao vya maendeleo katika jamii,”amesema.
Hata hivyo ametoa rai kwa wananchi na vijana kujitokeza kushiriki katika maadhimisho ya wiki hiyo ya vijana inayofanyika Viwanja vya Furahisha kuanzia Oktoba 8-13, 2024 na Kilele cha Mbio za Mwenge kitakachofanyika Uwanja wa CCM Kirumba Oktoba 14, 2024.
0 Comments