Header Ads Widget

JITIHADA ZA RAIS SAMIA KUTANGAZA UTALII ZAONGEZA IDADI YA WATALII RUAHA

 

Na Matukio Daima media

JITIHADA za Rais Dkt Samia Suluhu Hassan za kutangaza utalii kupitia filam ya The Royal Tour zimeongeza idadi ya watalii katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha imeongezeka  kutoka wastani wa watalii 5,320 mwaka mwaka 2001/2002 hadi kufikia 19,932 mwaka 2023/2024.

Akifungua kongamano la Miaka 60 ya Hifadhi ya Taifa ya Ruaha Leo  katika ukumbi wa Royal Palm mjini Iringa  kwa niaba ya mkuu wa mkuu wa mkoa wa Iringa Peter Serukamba,Mkuu wa Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya  Kanal Maulid Hassan Surumbu.

Alisema kuwa hifadhi hiyo imeona ukuaji mkubwa katika sekta ya utalii, ambapo idadi ya watalii imeongezeka kwa kiwango Kikubwa zaidi .


 Surumbu alisifu juhudi za Rais Samia Suluhu Hassan katika kufungua nchi na kuimarisha utalii wa Tanzania duniani kote.

Alisema kuwa hifadhi hiyo imeona ukuaji mkubwa katika sekta ya utalii na kupitia ukuaji huo Hifadhi ya Ruaha imeendelea kuwa kimbilio la watalii wa ndani na nje.
 
Pia alipongeza ushirikiano mzuri kati ya hifadhi hiyo na jamii zinazozunguka kupitia mpango wa ujirani mwema, ambao umeimarisha mahusiano na kusaidia katika kupunguza uhalifu.

"Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan imekuwa ikifanya  juhudi za dhati za kuboresha sekta ya utalii na kufungua utalii wa ukanda wa Kusini Nitumie fursa hii kwa namna ya pekee kuwashukuruku TANAPA kupitia Hifadhi ya Taifa Ruaha kwa kuona umuhimu wa kufanya kongamano hili la kuadhimisha miaka 60 toka Hifadhi ilipoanzishwa" 


Alisema Katika kipindi cha miaka 60, Hifadhi ya Taifa Ruaha imepitia vipindi vya mabadiliko mbalimbali kutokana na mabadiliko ya Sera na miongozo ya nchi, mabadiliko ya asili, kukua kwa teknolojia, na changamoto za mabadiliko ya tabia nchi.

 Hata hivyo, pamoja na mabadiliko haya Serikali imefanya kazi kubwa kuhakikisha shughuli za uhifadhi zinafanyika kwa weledi mkubwa Mathlani, mwaka 2008 Serikali ilifanya juhudi za makusudi za kubadili mipaka ya Hifadhi ya Taifa Ruaha kwa kuongeza sehemu ya bonde la Usangu.

" Lengo likiwa kutunza vyanzo vya Mto Ruaha Mkuu kwa lengo la kuunusuru Mto huo na changamoto za kukauka mara kwa mara ili kupata maji ya kutosha kwa ajili ya wanyamapori na bwawa la umeme la Mtera, na sasa bwawa kubwa la Mwalimu Nyerere"


Alisema Changamoto kubwa ya Hifadhi na mfumo wa ikolojia wa Ruaha ni ujangili wa nyamapori na meno ya tembo.

Alisema  takwimu za sensa ya wanyamapori katika mfumo ikolojia wa Ruaha iliyofanyika mwaka 1977 lilihesabu takribani tembo 40,000. 

Hata hivyo idadi ya tembo iliendelea kupungua hasa miaka ya 1980 wakati ambapo biashara ya meno ya tembo ilishamiri nchini. 

Alisema hadi kufikia mwaka 1993 idadi ya tembo kwenye mfumo Ikolojia wa Ruaha ilikadiriwa kuwa 18,864 idadi iliyoendelea kupungua kupungua na kufikia wastani wa tembo 15,521 mwaka 2018. 

Kupitia Sensa iliyofanyika mwaka 2021 imeonesha kuendelea kuboresha sekta ya utalii na kufungua utalii katika hifadhi za kusini. 

Mbunge wa Iringa Mjini, Jesca Msambatavangu, alisisitiza kuwa chini ya serikali ya awamu ya sita, sekta ya utalii imeendelea kukua na kuleta maendeleo ya kiuchumi mkoani Iringa. 

Ameeleza juhudi za serikali kuboresha miundombinu kama vile upanuzi wa uwanja wa ndege na ujenzi wa barabara ya lami ya Iringa - Msembe, ambazo zinatarajiwa kukuza zaidi sekta ya utalii na kutoa fursa za kiuchumi kwa wakazi wa mkoa huo.

Msambatavangu pia alisema upo  umuhimu wa kulinda tembo, akieleza kwamba idadi yao duniani imepungua kwa kasi, na sasa ni muhimu kwa wananchi wa Iringa kuwahifadhi ili kuendeleza utalii. 

Amewataka wakazi kuchangamkia fursa za kituo cha utafiti wa wanyama pori kinachojengwa Kihesa, Kilolo, ili waweze kujifunza na kuishi kwa amani na wanyama.


Akielezea jitihada za Kulinda Hifadhi ya Ruaha pamoja na mto Ruaha mkuu,Mkuu wa hifadhi ya taifa ya Ruaha, Godwell Ole Meing'ataki alisema mto Ruaha umekuwa na historia ya kukauka kila mwaka ifikapo kipindi cha kiangazi kwa miezi miwili hadi sita wakati mwingine, jambo ambalo linaathiri wanyama, ndege na mazingira ya hifadhi hiyo.

Meing'ataki aliongeza kuwa licha ya kuathirika kwa viumbe na hifadhi, ukaukaji wa mto huo unaathari kubwa kwa binadamu kwani maji ya mto ruaha yanatumika pia katika shughuli mbali mbali ikiwemo uzalishaji wa umeme katika Bwawa la Mtera, Kidatu, bonde la Kilombero na mto mkuu Rufiji pamoja na shughuli za kilimo na kijamii.

"Historia ya huu Mto umekuwa na changamoto ya kukauka, maji kupungua na kuacha kutiririka kabisa lakini tunashukuru mwaka mpaka tarehe hizi maji bado yanatiririka, lakini inawezekana baada ya miezi miwili ijayo ndani ya miezi miwili ijayo, kama mvua hazitanyesha unawezakukauka kabisa", Alisema Meing'ataki.

"Mto huu umekuwa unakauka kwa kipindi cha miezi miwili mpaka miezi sita wakati mwingine kulingana na Mvua lakini pia kulingana na au kutokana na matumizi mbali mbali huko kwenye nyanda za juu ambapo mito inaanzia, ambako inaingiza maji yake kwenye mto Ruaha, kwa hiyo hii changamoto imekuwepo kwa muda mrefu sana ni zaidi ya miaka 35 mto huu umekuwa unakauka kwa kipindi cha kiangazi unakauka na kuleta madhara makubwa kwa mazingira ya hifadhi, lakini pia tunafahamu kwamba huu mto pamoja na kuwa ni sehemu muhimu ya uhai wa hifadhi ya taifa ya Ruaha"



Hivyo alisema Kwa kuwa  ndicho chanzo kikuu cha maji kwa ajili ya wanyama, ndege, mimea na mazingira lakini pia huu mto unatumiwa na binadamu kwaajili shughuli mbali mbali unapotoka nje ya hifadhi, hasa kule katika maeneo ya Mtera mnafahamu kuna uzalishaji wa umeme, baada ya Mtera tuna pia Kidatu umeme pia unazalishwa, lakini  mto huo unapitisha maji yake kupeleka kule kwenye bonde la Kilombero na hatimaye kwenda kwenye mto mkuu Rufiji ambapo kule tuna mradi mkubwa wa uzalishaji umeme wa Mwalimu Nyerere.

Alisema  mto huo unachangia maji yake katika maeneo haya, lakini pia huu mto unatumika katika shughuli zingine za kilimo, na zile za kawaida za nyumbani, shughuli za kijamii, uvuvi pia unafanyika na ufugaji kwa hiyo mto huu una mchango mkubwa katika maeneo mbali mbali na katika nchi .

Aidha, Meing'ataki alisema mto Ruaha mkuu umeanzia ndani ya hifadhi hiyo katika eneo la Usangu Kuna chanzo halisi cha maji ya mto huo yakitokea nje ya hifadhi katika maeneo mbali mbali ya nyanda za juu kusini Ikiwemo Chunya, Makete, Hifadhi ya Kitulo, Pori la akiba Mpanga, Wanging'ombe na Mufindi.

"Mto huu unaanzia ndani ya Hifadhi kwa maana ya The Great Ruaha River katika eneo la Usangu ambalo liko ndani lakini chanzo halisi cha maji ya mto Ruaha nje ya hifadhi katika maeneo mbali mbali ya nyanda za juu kusini hasa mkoa wa Mbeya Ikiwemo wilaya ya Chunya, wilaya Makete, Hifadhi ya Kitulo, Pori la akiba Mpanga, na maeneo mengine ya wilaya ya wanging'ombe na Mufindi.


Alisema mto huo ni rasilimali kwa Hifadhi ya taifa ya Ruaha kwani uoto wa asili, wanyama, ndege na viumbe vingine vyote vinategemea maji ya mto huo, hivyo kukauka kwa mto huo kunaathari kubwa kwa hifadhi hiyo ikiwemo kufa kwa wanyama wanaoishi katika mto huo.

Kuhusu  changamoto ya ujangili katika hifadhi hiyo alisema kuwa kumekuwepo na  baadhi ya watu ambao hutumia silaa na wengine hutumia sumu kwa kuweka katika maji ya mto Ruaha ili kuuwa mnyama ama samaki bila kujali madhara yanayobakia kwa viumbe vingine vitakavyotumia maji hayo, jambo ambalo limekuwa na athari kubwa kwa viumbe hai wa hifadhi na watumiaji pia.

"Ni kitu kibaya sana kuzungumza hivyo, lakini ni kweli kwamba kuna baadhi ya watu wanatumia sumu kuulia wanyama hata kwenye samaki tunaona wanatumia sumu, tunakuta mabaki ya zile sumu na tumethibitisha kwenye maabara pia, kwa hiyo zile nyama na wale samaki wanachukuliwa ni dhahiri wananchi wanapelekwa kuuziwa kwenye maeneo yao, kwa hiyo mara nyingi tukifika kwenye jamii tumekuwa tukitoa elimu na kuwaambia wache tabia ya kula nyama pori ambazo hazijathibitishwa kwani zinaweza kuwa na sumu" alisema Meing'ataki.


Hata hivyo alisema katika kuadhimisha miaka 60 ya hifadhi hiyo, imekuja wakati ambao taifa likiwa na historia kubwa katika sekta ya utali baada ya kuandaliwa filamu kubwa ya the royal tour ambayo imefanywa na rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, hivyo kuitaka jamii kuunga mkono juhudi hizo ili kuendelea kunufaika na hifadhi hiyo.

Alisema katika maadhimisho hayo wamejipanga kuendelea kutoa elimu kwa jamii umuhimu wa rasilimali hizo kwa na kwa vizazi vijavyo.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI