Header Ads Widget

HATIMAYE NEYMAR AREJEA UWANJANI BAADA YA MWAKA MMOJA

 


NA MATUKIO DAIMA MEDIA SAUDI ARABIA 

NEYMAR ameonekana kwa mara ya kwanza dimbani katika kipindi cha mwaka mmoja, akitokea benchi katika kipindi cha pili cha mchezo wa Ligi ya Mabingwa Asia wakatil AFC Al Hilal iki- ivaa Al Ain.


Nyota huyo wa Brazil alichukua na- fasi ya Nasser Al Dawsari dakika ya 77, mara tu baada ya Salem Al Dawsari kufunga bao na kuifanya Al Hilal kuwa mbele kwa mabao 5-3.


Alikaribia kufunga bao akibadilis- hana pasi na Aleksandar Mitrovic ili kutengeneza nafasi kabla ya kupiga shuti lake nje kidogo ya lango.


Mchezo huo ulimalizika kwa Al Hilal kushinda mabao 5-4 baada ya Al Ain yenye maskani yake Falme za Kiarabu kufunga penalti ya dakika za mwisho.


Baada ya mchezo huo, Neymar alise- ma: Ninajisikia vizuri... huwa nina timu nzuri. Nina furaha sana. Nimere- jea!".


Mchezaji huyo wa zamani wa Paris Saint-Germain, alipata jeraha la goti wakati wa mechi ya kufuzu Kombe la Dunia ya Brazil dhidi ya Uruguay muda mfupi baada ya kujiunga na Ligi ya Sau- dia na alifanyiwa upasuaji Novemba mwaka jana.



Neymar alijiunga na Al Hilal Agosti 2023 akitokea PSG kwa uhamisho wa euro milioni 90, lakini alicheza mechi tano tu kabla ya kutumia .

Klabu ya zamani ya Neymar, Santos ilimpongeza mchezaji huyo kwa kure- jea kwenye chapisho lake katika uku- rasa wa X.

„Ilikuwa ni zaidi ya miezi 12 mbali na uwanja, na hamu kubwa ya kurudi kufanya kile anachopenda sana," klabu hiyo ya Brazil iliandika.


„Neymar si nyota tu. Si fikra tu. Ney- mar ni sawa na furaha katika soka. Kurejea kwake ni furaha ya mamilioni ya mashabiki duniani kote."

Fowadi huyo, ambaye ndiye mfungaji bora wa muda wote wa Brazil, alikosa michuano ya Copa America ya 2024 ambayo ilinyakuliwa na Argentina.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI