KATIKA Kuhakikisha ukatili wa kijinsia ndani ya jamii ya mkoa wa Iringa na Tanzania unakomesha mdau wa maendeleo Kilolo Aidan Mlawa amepongeza jeshi la Polisi mkoa wa Iringa chini ya RPC Alan Bukumbi kuzindua dawati la jinsia na watoto kuwa na kuunga mkono jitihada za Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa vitendo .
Kuwa ni jitihada za kuhakikisha ustawi wa watoto na vijana kupitia dawati hilo, lililozinduliwa na Mkuu wa Mkoa wa Iringa Peter Serukamba ni ukweli kuwa ni ulinzi tosha wa usalama wa watoto na vijana dhidi ya ukatili wa kijinsia pamoja na athari za utandawazi.
Mlawa amesema kuwa uzinduzi huo ni hatua muhimu katika kupambana na changamoto za kijamii kama mmomonyoko wa maadili, matumizi ya dawa za kulevya, ulevi, na mapenzi ya jinsia moja.
Amesema kuwa dawati hilo litaleta suluhisho kwa changamoto zinazowakumba vijana kwa kuimarisha maadili na kuhakikisha watoto wanalelewa katika mazingira salama.
Mlawa amesema kuwa uzinduzi wa dawati hili si jambo la kawaida, bali ni sehemu ya mkakati wa kitaifa wa kulinda haki za watoto na kuimarisha usawa wa kijinsia.
Amesema kuwa kuna ongezeko la visa vya ukatili wa kijinsia miongoni mwa watoto na vijana katika mikoa mingine japo Iringa hali si kubwa hivyo jambo linalohitaji hatua madhubuti na za haraka kutoka kwa wakati serikali na wadau wa maendeleo.
"Kama wadau wa maendeleo, tunapaswa kushirikiana na taasisi za umma kama vile dawati hili ili kuhakikisha kila mtoto analindwa dhidi ya vitendo vya ukatili na madhara ya utandawazi.
Hii ni dhamira muhimu kwa ajili ya kujenga kizazi chenye maadili na uadilifu," alisema Mlawa.
Dawati la Jinsia na Watoto linalenga pia kusaidia familia kujenga mifumo madhubuti ya mawasiliano na malezi bora ili kuhakikisha watoto wanalelewa katika misingi ya maadili mema.
Kupitia dawati hili, jamii inahimizwa kushirikiana na shule na vyombo vya usalama ili kufuatilia na kuzuia matendo yanayoweza kuhatarisha usalama wa watoto.
Aidan Mlawa amesema kuwa familia inapaswa kuwa ngome ya kwanza katika kupambana na changamoto za mmomonyoko wa maadili.
Alisema kuwa mabadiliko ya kijamii na tamaduni zisizofaa zimekuwa changamoto kubwa kwa vijana wa sasa, hivyo juhudi za makusudi zinahitajika katika kuwafundisha maadili mema na kuwaelekeza kwenye njia sahihi.
“Hatuwezi kuiachia serikali pekee jukumu la kuwalinda watoto na vijana wetu. Kila mzazi na mlezi ana wajibu wa kushiriki katika malezi yenye misingi ya maadili thabiti. Lazima tuwaambie mapema kabla hawajaharibiwa,” alisema Mlawa akirejelea ujumbe wa kampeni mpya ya Mkoa wa Iringa inayojulikana kama “Tuwaambie Kabla Hawajaharibiwa.”
Kampeni hii iliyozinduliwa sambamba na dawati la jinsia inalenga kutoa elimu ya mapema kwa watoto na vijana kuhusu madhara ya tabia hatarishi kama vile dawa za kulevya, ulevi, na mienendo isiyofaa. Mlawa aliipongeza kampeni hiyo akisema kuwa itasaidia kupunguza vitendo vya ukatili wa kijinsia na tabia zisizofaa katika jamii.
Alibainisha kuwa kampeni kama hizi ni muhimu katika kuimarisha kizazi chenye maadili na kuhakikisha vijana wanakuwa raia wema na wachangiaji wazuri wa maendeleo ya taifa. “Kuwajenga watoto na vijana kimaadili ni msingi wa mafanikio ya taifa lolote.
Lazima tuwekeze katika elimu ya maadili na kuwalinda watoto wetu mapema,” aliongeza Mlawa.
Mlawa aliwahimiza wadau wa maendeleo kushirikiana kwa karibu na Jeshi la Polisi, hasa Dawati la Jinsia, ili kuhakikisha sheria zinazingatiwa na wahusika wa ukatili wanachukuliwa hatua.
Alitoa pongezi kwa Jeshi la Polisi Mkoa wa Iringa kwa juhudi zao za kuongoza kampeni za kuelimisha jamii na kushughulikia malalamiko ya watoto na wanawake wanaokumbwa na ukatili.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, RPC Allan Bukumbi, alisisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya familia na dawati hilo kwa kusema.
“Familia zinapaswa kuwa mstari wa mbele katika kuzuia mmomonyoko wa maadili, huku dawati la jinsia likitoa msaada pale unapoonekana kuna dalili za ukiukwaji wa haki za watoto.”
Mlawa aliitaka serikali na wadau wa elimu kuimarisha ushirikiano na shule za msingi na sekondari katika kuelimisha wanafunzi kuhusu madhara ya ukatili wa kijinsia na tabia hatarishi.
Alitoa mfano wa shule zilizoonyesha mfano mzuri katika ushiriki wa masuala ya kijamii, akitaja Luindo Pre and Primary School ,na nyingine zilizoshiriki kutoa vyombo vya usafiri Leo kama mfano bora wa taasisi inayoshiriki kikamilifu katika masuala ya kijamii.
"Shule zina nafasi kubwa ya kuwafundisha watoto siyo tu masomo ya darasani, bali pia maadili na heshima kwa kila mmoja. Tunapaswa kuzitumia taasisi hizi kwa manufaa ya watoto wetu," alisema Mlawa.
Aidan Mlawa alihitimisha kwa kuipongeza serikali ya Mkoa wa Iringa kwa kuzindua Dawati la Jinsia na Watoto pamoja na kampeni ya "Tuwaambie Kabla Hawajaharibiwa."
Alisisitiza kuwa mafanikio ya kampeni hii yanahitaji ushirikiano wa kila mmoja – kutoka kwa wazazi, walimu, viongozi wa dini, na mashirika ya kiraia.
Kwa kushirikiana kwa karibu, alisema Mlawa, tunaweza kujenga jamii yenye maadili mema na kuhakikisha kuwa watoto na vijana wanakuwa salama na wanapata malezi bora. "Hili ni jukumu letu sote.
Tukilinda kizazi hiki, tunajenga msingi wa taifa lenye mafanikio na maadili thabiti kwa siku zijazo," alihitimisha Mlawa.
Dawati la Jinsia na Watoto linalenga kuwa sehemu muhimu ya juhudi za mkoa wa Iringa katika kuimarisha usalama wa kijinsia na malezi bora.
Kampeni ya “Tuwaambie Kabla Hawajaharibiwa” pia inatoa matumaini ya kuwaelimisha vijana mapema na kuzuia athari za tabia zisizof
0 Comments