Header Ads Widget

ZAIDI YA EKARI 500 KUWANUFAISHA VIJANA WA BBT WILAYA YA NJOMBE

 


Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE


Zaidi ya ekari 500 zinazofaa kwa kilimo cha mazao mbalimbali wilayani Njombe zimetakiwa kupimwa kwa ajili ya  vijana kupitia mradi wa Jenga kesho iliyobora BBT ambao wanatarajia kupata mkopo wa riba ya asilimia 4 pindi watakapovuna.


Wizara ya Kilimo kupitia mradi huo imetembelea na kukagua baadhi ya mashamba ambapo mkuu wa wilaya ya Njombe Kissa Kasongwa anawataka vijana hao kutobweteka na badala yake watumie fursa hiyo huku akilaani tabia za baadhi ya vijana walioanza kubeza programu hiyo.


Mratibu wa mradi wa BBT Toka wizara ya Kilimo Vumilia Zinkakuba anasema Tanzania imekuwa na fursa nyingi ambazo vijana wanashindwa kuzitumia hivyo kupitia mradi huo uwasaidie kujikwamua kiuchumi.


Naye Mkurugenzi mtendaji wa Mfuko wa Pembejeo toka Wizara ya Kilimo Mwanahiba Mzee amewataka vijana walioomba mkopo wa Kilimo kufanya marekebisho ya maombi yao ili yaendane na uhalisia wa mradi wanaotaka kufanya kwani fursa bado zipo.



Kwa upande wao baadhi ya vijana akiwemo Yuda Gurty na Martha Mwindi wanakiri kuwa mradi huo unaweza kuwapa manufaa endapo watautekeleza huku wakiiomba serikali kuwasaidia ili wapate mikopo hiyo.


Mamia ya vijana waliokosa ajira wanaanza kuiona fursa kupitia mradi wa Jenga kesho Iliyobora ulioanzishwa na mkuu wa wilaya ya Njombe huku serikali kwa ngazi ya Halmashauri ikilazimika kuanza kutekeleza katika mkoa wa Njombe kwa kuwa wameiona fursa mapema kuliko mikoa mingine.







Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI