Na Pamela Mollel,Arusha
Waziri wa mipango na uwekezaji profesa Kitila Mkumbo anatarajiwa kufungua maadhmisho ya wiki ya azaki mwaka 2024 itakayoshirikisha zaidi ya washiriki mia sita kutoka sekta binafsi,serikali na wadau wa maendeleo itakayofanyika kuanzia tarehe 9 hadi September 13 jijini Arusha.
Akizungumza na waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari Mkoani Arusha,Mkurugenzi mkazi wa CBM International na Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya wiki ya Azaki,Nesia Mahenge anasema watu zaidi ya 600 wanatarajiwa kushiriki pamoja na mashirika zaidi 400 kutoka ndani na nje ya Nchi
Anasema kuwa wiki hiyo ya azaki inajumuisha Azaki zote za kiraia ambazo zinashughulika katika maendeleo ya nchi ikiwa ni pamoja na kuwepo kwa balozi wa Canada
Naye , Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Foundation for Civil Society (FCS), Justice Rutenge, anasema wiki hiyo imebebwa na kaulimbiu isemayo; Sauti, Dira na Thamani ikiendana na wakati uliopo na matukio yanayoendelea nchini, ambayo ni ya uchaguzi wa serikali za mtaa utakaofanyika mwaka huu, uchaguzi mkuu wa mwakani na uandaaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025-2050.
Aidha ameongeza kuwa, wiki hiyo pia itakuwa na mijadala mbalimbali inayohusu shughuli za AZAKi nchini, maendeleo ya jamii na ushirikiano baina ya asasi za kiraia, serikali na sekta binafsi.
Maadhimisho ya wiki ya AZAKi 2024 ni ya sita kufanyika tangu kuanzishwa kwake mwaka 2018.
Hata hivyo Zaidi ya vijana 70 wanatarajiwa kushiriki katika wiki hiyo ambapo watapata fursa ya kuweza kujifunza maswala mbalimbali juu ya ushiriki wao katika demokrasia na namna wanavyotakiwa kushiriki katika shughuli za ujenzi wa Taifa
“ Mahenge .
ameongeza kuwa ,kupitia maadhimisho hayo ambayo kufanyika kila mwaka yameleta mafanikio makubwa sana kutokana na wananchi kuweza kujifunza maswala mbalimbali kutoka kwa wengine
"
Kwa upande wake Mkuu wa kitengo cha sekta za umma kutoka benki ya Stanbic , Doreen Dominic amesema kuwa,wamekuwa wakifanya wiki hiyo kwa mfululizo mwaka wa sita sasa huku lengo kubwa likiwa ni kupaza sauti ya pamoja katika maswala mbalimbali .
Ameongeza kuwa,kupitia wiki hiyo wanaungana na taasisi mbalimbali katika kufanya maboresho mbalimbali na kujadili sauti ya pamoja na kuhakikisha wanapigania haki za watanzania wote waliopo katika maeneo mbalimbali ili waweze kupata haki zao za msingi .
Mkurugenzi wa Haki elimu ,John Kalaghe amesema kuwa kupitia wiki hiyo kutakuwepo na kipindi cha vijana ambapo wataweza kushiriki kikamilifu na kujadili juu ya ushiriki wao katika kuandaa majadiliano kwa vijana juu ya nafasi zao na ushiriki wao katika nafasi mbalimbali.
Mkurugenzi wa Mtandao wa jinsia Tanzania Tanzania (TGNP),Lilian Liundi amesema kuwa,zaidi ya waandaaji 20 kutoka asasi za kiraia wakishirikiana katika kuandaa wiki hiyo ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ni sauti,dira na dhamani.
"Zaidi tunataka sauti za wananchi iweze kusikika
Kwa kuwa kuna umuhimu mkubwa wa kuweka sauti za wadau wote"anasema Liundi
0 Comments