Header Ads Widget

WANANCHI KATA YA MAENDELEO WALIA NA UKOSEFU WA ZAHANATI, MAJI NA KERO YA BARABARA.

 

NA JOSEA SINKALA, MBEYA.

Wananchi wa vijiji vya Izumbwe na Ikokho kata ya Maendeleo Mbeya vijijini wameitaka Serikali kutatua kero ambazo bado ninawakabidhi ikiwemo umaliziaji zahanati ambayo inadaiwa kutokamilika kwa muda miaka minane.



Akizungumza kwenye mkutano na Mbunge wa Mbeya vijijini, mmoja wa wananchi wa kijiji cha Izumbwe, amesema wananchi walianza kujenga zahanati ni mwaka wa nane sasa bado haijafunguliwa.


Pia wananchi hao wametaka kuharakishwa kujengwa mradi wa maji kwenye kijiji na kata yao ili kusogeza karibu huduma ya maji.


Pamoja na kero hizo pia wameeleza kukabiliwa na miundombinu mibovu  ya barabara ya kutoka Izumbwe msituni kuunganisha na barabara ya lami katika kijiji cha Ikokho ambayo haijawahi kulimwa na imekuwa korofi hasa kipindi cha masika.



Akijibia kero hizo Mbunge wa Mbeya vijijini Mhe. Oran Njeza ameahidi kuendelea kuwapigania kuhakikisha huduma hizo zinatatuliwa kama ilivyokuwa kwenye barabara ya lami ambayo iliahidiwa kutoka Inyala kupita Ikokho hadi Tembela na sasa ilishakamilika pamoja na miradi mbalimbali.


Kaimu meneja wa Wakala wa maji vijijini RUWASA Mhandisi Modestus Chingwile, amesema Serikali kupitia wataalam wa maji wana mpango wa kujenga tank na dakio la maji kwa ajili ya kijiji cha Ikokho hivyo kuwaondoa hofu.


Naye kaimu meneja wa Wakala wa barabara mjini na vijijini TARURA wilayani Mbeya Mhandisi Arcad Tesha amesema barabara ya Izumbwe itaingizwa kwenye bajeti kwa mwaka ujao wa fedha ili ijengwe pamoja na daraja lake.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI