Na Matukio Daima App
SERA ya Elimu ni mwongozo unaowekwa na serikali kuendesha na kuboresha sekta ya elimu nchini.
Sera hii inajumuisha malengo, mikakati, na taratibu zinazolenga kuhakikisha elimu bora kwa wananchi wote ,Sera hii inalenga kukuza upatikanaji wa elimu kwa wote, kuimarisha ubora wa ufundishaji na ujifunzaji, na kuhimiza maendeleo ya kiteknolojia na ujuzi wa kisasa.
Pia inahakikisha usawa wa kijinsia, kupunguza umaskini kupitia elimu, na kuandaa wanafunzi kuwa raia wenye uwezo wa kuchangia maendeleo ya taifana Mabadiliko ya sera yanazingatia changamoto za sasa na mahitaji ya jamii.
Katika miaka ya hivi karibuni, shule za St. Dominic Savio, zilizoko mkoani Iringa, zimekuwa kivutio kikubwa kwa wazazi na walezi wanaotafuta elimu bora kwa watoto wao.
Shule hizi, ambazo zilianza mwaka 2005, zimejipambanua kwa kutoa elimu yenye viwango vya juu na kujenga mazingira bora ya kujifunzia.
Ukuaji wa shule hizi na sifa zake za kipekee umekuwa mojawapo ya sababu kuu zinazowafanya wazazi wengi kuwapeleka watoto wao huko.
Shule za St. Dominic Savio zilianza kama taasisi ndogo ya elimu na madarasa machache, lakini zimekuwa na mafanikio makubwa.
Kwa kuanzia na wanafunzi 250 pekee, sasa shule hizi zinahudumia zaidi ya wanafunzi 3,068 katika matawi manne tofauti ya shule za awali na msingi, yakiwemo St. Dominic Savio Main Campus, St. Dominic Savio Mkimbizi, St. Dominic Savio Kigonzile, na St. Dominic Savio Ngelewala.
Ukuaji huu wa haraka unaweza kuelezwa na mikakati mizuri iliyowekwa na uongozi wa shule pamoja na nia yao ya kutoa elimu bora.
Mkurugenzi wa shule hizo Father Aidan Ulungi anasema kuwa shule hizi zimeanzisha matawi ya sekondari kama vile St. Dominic Savio Sekondari (Tosamaganga), St. Dominic Savio Kigonzile Sekondari, na Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Cagrielo.
Kuwa hivyo inafanya shule hizi kuwa na mtandao mpana wa elimu, unaowezesha wanafunzi wanaohitimu elimu ya msingi kuendelea na masomo yao ya sekondari katika mazingira yale yale bora waliyoyazoea.
Sababu Zinazozifanya Shule za St. Dominic Savio Kuwa Kimbilio la Wazazi Kuna sababu mbalimbali zinazoifanya shule hizi kuvutia wazazi wengi Ubora wa Kitaaluma moja ya sababu kuu zinazowafanya wazazi kupeleka watoto wao St. Dominic Savio ni ubora wa kitaaluma wa shule hizi.
Anasema kuwa wnafunzi wa shule hizi wamekuwa wakifanya vizuri sana katika mitihani ya kitaifa, huku wakiwa wanashika nafasi za juu kimkoa na kitaifa.
Kwa mfano, shule hizi zimeendelea kuongoza kimkoa na kiwilaya kwa muda wa miaka kadhaa.
Kuwa Shule zimeweka mikakati mizuri ya kuwajenga wanafunzi kitaaluma kupitia mazoezi ya mitihani mbalimbali ya ndani na nje, kama vile mitihani ya wathibiti ubora wa shule, Mock kata, Mock wilaya, na Mock Mkoa.
Kuhusu Teknolojia ya Kisasa St. Dominic Savio imewekeza sana katika matumizi ya teknolojia za kisasa kufundishia na kujifunzia.
Shule zinatumia vifaa vya kidigitali kama vile kompyuta, projekta, na vishikwambi, ambavyo vinasaidia wanafunzi kujifunza kwa urahisi zaidi.
Miradi ya teknolojia kama PROFUTURO, TESEA, na E-Learning imewekwa ili kuwapa wanafunzi uwezo wa kufikia maarifa na taarifa kwa njia rahisi zaidi, hali inayoifanya shule hizi kuwa na mazingira bora ya kufundishia.
Pamoja na elimu bora, shule za St. Dominic Savio zimejikita katika kuwajenga wanafunzi kwa misingi ya maadili na nidhamu.
Anasema kuwa watoto wanapewa malezi bora, yanayochangia si tu katika ufaulu wao kitaaluma, bali pia katika kuwa na tabia njema.
"Hii ni sifa inayowavutia wazazi wengi, kwani wanajua kuwa watoto wao watapata elimu iliyo bora, pamoja na maadili mazuri"
Baadhi ya wahitimu wakiwa katika ibada takatifu Siku ya Mahafali ya shule za St Dominic Savio Iringa picha na Matukio Daima App Shule za St. Dominic Savio zimejipambanua wazi kwa kuzingatia mipango bora ya kielimu inayolenga kuleta matokeo chanya kwa wanafunzi.
Walimu wamekuwa wakifanya kazi usiku na mchana kuhakikisha kuwa wanafunzi wanapata maarifa na ujuzi unaohitajika pia Wanafunzi wanapata fursa ya kufanya mitihani ya majaribio mara kwa mara, ambayo inawasaidia kujiandaa vizuri kwa mitihani ya mwisho.
" Mipango hii imeleta matokeo mazuri katika mitihani ya kitaifa, na hivyo kuongeza mvuto kwa wazazi kuwaleta watoto wao"
Musa Myula ni mmoja wa wasaidizi wa wakurugenzi shule za St Dominic Savio anasema kuwa Changanoto ambayo inakabili shule ni tatizo la baadhi ya wazazi kutolipa ada kwa wakati, hali inayosababisha kuyumbisha mipango ya shule.
Baadhi ya wahitimu wa shule za St Dominic Savio wakiwa katika Mahafali yao.picha na Matukio Daima App
Kwani ada ni chanzo kikuu cha mapato kinachotumika kuendesha shule, hivyo ucheleweshaji wa ada unakwaza utekelezaji wa mipango mbalimbali.
Kuwa katika muktadha wa elimu ya Tanzania kwa sasa, viwango vya elimu vinaendelea kuboreka, na shule binafsi kama St. Dominic Savio zimechangia sana katika ukuaji huo.
Tanzania imekuwa ikifanya juhudi kubwa katika kuboresha elimu ya msingi na sekondari, na shule hizi zimekuwa mfano mzuri wa jinsi ubora wa elimu unavyoweza kuboreshwa kupitia mipango na mikakati bora.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda
Serikali imekuwa ikishirikiana na shule binafsi katika kuboresha viwango vya elimu, na shule za St. Dominic Savio zimekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha kwamba wanafunzi wanapata elimu bora.
Hivyo Shule hizi zimekuwa zikitoa mchango mkubwa katika kuongeza ushindani wa kitaaluma kati ya wanafunzi, hali inayochangia katika kuongeza ubora wa elimu nchini.
Aidha shule zimekuwa zikienda Sanjari na mpango wa Taifa wa TEHAMA kwani ongezeko la matumizi ya teknolojia katika shule hizi ni mfano mzuri wa jinsi teknolojia inavyoweza kutumika kuboresha elimu.FAHAMU ZAIDI KUHUSU ST DOMINIC SAVIO IRINGA BOFYA LINK HII
Anasema Serikali inapaswa kuhamasisha shule nyingi zaidi kutumia mifumo ya kidigitali kufundishia na kujifunzia kama vile inavyofanyika katika St. Dominic Savio, ili kuongeza tija kwa wanafunzi na walimu.
Panuel Sanga na Anna Siwonike ni baadhi ya wazazi ambao watoto Wao wamehitimu katika shule za St Dominic Savio wanapongeza ubora wa shule hizi na kutaka wazazi kulipa ada kwa wakati.
Kuwa Shule za St. Dominic Savio zimejipambanua kuwa miongoni mwa shule bora zaidi nchini Tanzania hivyo lazima wazazi walipe ada wasipende vitu vizuri bila kuvitolea jasho.
Aidha walisema ubora wa kitaaluma, matumizi ya teknolojia za kisasa, maadili na nidhamu, pamoja na mipango bora ya elimu, ni miongoni mwa sababu zinazowafanya wazazi wengi kuvutiwa na shule hizi.
Mbali ya changamoto hiyo shule hizi zimeendelea kukua na kutoa mchango mkubwa katika kuboresha viwango vya elimu nchini Kwa hakika, shule za St. Dominic Savio ni kielelezo cha mafanikio katika sekta ya elimu Tanzania, na zimeweka msingi mzuri wa kuwa na kizazi kilichoelimika na kinachozingatia maadili mema kwa watoto .
mkurugenzi wa shule za St Dominic Savio Father Aidan Ulungi katikati akiwa na baadhi ya Walimu wa shule hizo .picha na Matukio Daima App
KWA HABARI NA MAKALA MBALI MBALI ENDELEA KUFUATILIA MATUKIO DAIMA APP,MATUKIO DAIMA BLOG NA MATUKIO DAIMA TV (ONLINE) PIA MITANDAO YOTE YA KIJAMII NA USIKOSE KUSOMA GAZETI LA MWANAHABARI NA MACHINGA KILA SIKU IWAPO UNAHITAJI KUTANGAZA NASI PIGA SIMU 0754026299 EMAIL: matukiodaima3@gmail.com
0 Comments