Header Ads Widget

RC.SERUKAMBA ATIKISA SOKO KUU MAFINGA WAPO POLISI ,JWTZ NA UHAMIAJI.

Na Fredrick Siwale -Matukio Daima APP -Mufundi.                               

WAFANYABIASHARA wa Soko kuu Mafinga walitikisika kwa muda kufuatia ujio wa Mkuu wa Mkoa wa Iringa kuwatikisa ,kwa kuwaambia anavunja vibanda vyote 331 vya soko hilo.

Hayo yalijiri kufuatia kuwepo kwa mgogoro wa muda mrefu wa Soko  kuu vibanda vya zamani 331 na Wajenzi na  Halmashauri ya Mji Mafinga kuhusu upandaji wa Kodi ya Ardhi.                                  

Mhe.Peter Serukamba akiwa na timu yake ya kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa na Wilaya walifika Soko kuu Mafinga wakiwa kamili na kufanya mkutano wa hadhara na Wafanyabiashara eneo la ofisi ya Soko.                   

Katika hali isiyokuwa ya kawaida baada ya Mkuu wa Mkoa kueleza dhamira ya kufika sokoni hapo ukimya uliawala na hakuna aliyejibu chochote.

Kwa hiyo mmeambiana msijibu chochote!  Nauliza wangapi wamelipa Halmashauri Ile sh.80,000 ? Narudia nani amelipa ?                  Nabadilisha swali ! Nani mpangaji ? Alihoji Serukamba.                          

" Mumeamua kufanya dharau ! sasa nachukua hatua Mkurugenzi na OCD hakikisha mnapitisha utepe (riboni) Soko zima na jioni naleta brudoza navunja Soko lote." Alisema RC.Serukamba.        

Baada ya tamko hilo la kufunga utepe na kubomoa soko  Mkuu wa Mkoa Mhe.Serukamba kufunga kikao cha dharula na kuanza kuondoka baadhi ya Wafanyabiashara waliamua kumpigia magoti asibomoe  na akaridhia na kuanza nao mazungumzo .                       

Uamuzi uliochukuliwa ni kuanza mapatano na makubaliano upya nje ya mikataba ya sh.80,000 ya awali iliyogomewa na kuanza mapunguziano kwa njia ya mnada kati ya Mkuu wa Mkoa na Wafanyabiashara mmoja mmoja mlangoni kwake.                                   

Makubaliano ikawa ni kati ya Mfanyabiashara na Mkuu wa Mkoa kwa mtindo wa punguzo yaani wapo walioamliwa kulipa sh.50,000 kavu kwa mwezi, sh.60,000 kavu kwa mwezi na sh.70,000 kulingana na ukubwa wa kibanda.            

Mhe.Justus Kisoma Diwani Kata ya Boma kwa upande wake alisema alichokifanya Mkuu wa Mkoa ni kutaka kuichonganisha Serikali na Wananchi kwani Kodi aliyoipanga awali ya sh.80,000 na hii mpya kwa njia ya mnada siyo rafiki na Wafanyabiashara.                 

" Kodi hii ni kubwa na sijua Mh.Serukamba ametumia sheria ipi kukokotoa na kupata kiasi hicho na hasa ikizingatiwa soko hilo lipo katika kitalu kimoja na Vibanda vipya ambavyo wao wanalipa kupitia njia ya ubia wa Wajenzi na Halmashauri ya sh.50,000 kwa sh.25,000 kulipa Halmashauri na 25,000 kujifidia.                                    

" Lakini nguvu anayotumia Mkuu wa Mkoa ni kubwa kwani kufika na Vyombo vya Ulinzi na Usalama wakiwepo Polisi, JWTZ, Magereza na Uhamiaji ni kuwatishia Wananchi" Alisema Mhe. Kisoma.                

Mhe.Kisoma alisema kitendo cha Mkuu wa Mkoa kutumia nguvu kubwa badala ya kanuni na Sheria zinazoendesha Mamlaka za Halmashauri ni ukiukwaji wa Serikali hizo.                                      

" Mwandishi wa habari Mimi nimekuwa Mhanga wa maamuzi ya Mkuu wa Mkoa kwani kila alifika Mafinga kwenye mikutano yake ni lazima jina langu litajwe kwa ubaya ikiwa ni pamoja na kutishiwa Kisiasa " Alisema Mhe.Kisoma.

" Hivi karibuni ujio wa Mhe.Abballa Ulega  Waziri wa mifugo na uvuvi nilitishiwa kuwa najifanya kuwatetea Wananchi lakini CCM itashinda hata bila ya Madiwani "na kuonyesha kuanza kushughulikiwa kisiasa wazi wazi" Alisema Mhe.Kisoma.

Mhe.Kisoma aliendelea kufungua kuwa awali vibanda hivyo vilikuwa vikilipia Kodi ya Ardhi kati ya sh.3,000,6,000 na sh.9,000 kwa mwezi kulingana na makubaliano ya awali kati ya Wajenzi) Wamiliki wa vibanda na Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi kwa wakati huo. 

Baada ya kuzaliwa Halmashauri ya Mji Mafinga sekeseke inadaiwa ilianzia hapo kwa Mkurugenzi kutaka ufanyike mchakato wa kuboresha mapato kwa kuongeza gharama za upangishaji Ardhi .                

Upande wake Bw .Filinus Mgaya Mwenyekiti wa Soko kuu Mafinga ambaye alisema mazungumzo ya awali kati ya Halmashauri kupitia Baraza la madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi chini ya aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji Bw.Limbakisye Shimwela ( Mandevu) kwa wakati huo yalikwenda vizuri sana.

" Mwandishi kila zama na wakati wake na kila shetani na mbuyu wake na zimwi likujualo halikuli ukakwisha na ndicho kilichotukuta Utawala wa Mkuu wa Wilaya Dkt.Linda Salekwa na Mkuu wa Mkoa Mhe.Peter Serukamba" Alisema Bw.Mgaya.

" Tangu kuteuliwa Viongozi hawa Wawili sokoni pamechimbika Kodi zinapangiwa majukwaani  kama biashara ya mnada huku na Vyombo vya Ulinzi na Usalama vikisimamia hadi tunatishika" Alisema Bw.Tenusi Msemwa .                          

Bw.Tenusi Msemwa alisema Wafanyabiashara wao walivijenga vibanda hivyo na wengine kuachiwa urithi na Wazazi wao zaidi ya miaka 30 iliyoyopita na wamekuwa walipa leseni  za biashara, Kodi za  TRA na mapato ya Halmashauri kwa makubaliano yao kwa maandishi na hakukuwa na mgogoro wowote.           

" Naomba ikumbukwe baada ya Utawala wa sasa kuanza ulikuta mchakato unaendelea wa kutwaliwa vibanda hivyo vya zamani kupitia Halmashauri ya Mji Mafinga na Wafanyabiara (Wajenzi) wa kuingia ubia kwa kusimamiwa na ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mhe.Halima Dendego wakati huo ambaye alihamishwa" Aliongeza kusema Bw.Msemwa.      

Alisema mazungumzo yalikuwa yamefikia mahali pazuri kwani tayari suala hilo lilikuwa mezani kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji Bw.Ayoub Kambi kwa wakati huo..         

" Njia ilianza kuonekana kwani Baraza la madiwani Halmashauri ya Mji Mafinga walifikia maamuzi ya kuwa tuingie ubia wa kwa kulipa sh.50,000 kwa mwezi ambapo Halmashauri ingelipwa sh.25,000 na Wafanyabiashara kujikata 25,000 kama fidia ya Ujenzi kwa kipindi cha miaka 14 na Vibanda kuwa mali ya Halmashauri na Wajenzi kurudi kuwa Wapangaji " Alisema Bw.Msemwa.          

Bw.Msemwa Uamuzi huo ulifikiwa baada ya kuona wenzao walijenga vibanda vipya wao wanalipa sh.50,000 ikiwa sh.25,000 wanalipa Halmashauri na sh.25,000 wanajikata kufidia gharama za Ujenzi wa vibanda hivyo.   

"Wakati wenzetu  wanapeta kwa kulipa sh.25,000 kwa mwezi Halmashauri kwa kibanda ambacho na wao wanapangisha kati ya sh.250,000 ,150,000 na sh.100,000 kwa mwezi vibanda vya zamani tunalazimishwa kulipa sh.80,000 kwa mwezi mwezi tena bila kufidiana haki Iko wapi" Alisema Bw.Msemwa.       

 Vibanda vipya nguvu yao ni kwamba wajenzi ni Halmashauri yenyewe kupitia benki ya Dunia na vingine vimejengwa na Watumishi wa Serikali ngazi ya Wilaya waliopo na Waliohama na msimamizi Mkuu na mpangishaji wa sh.250,000 na 150,000 ambaye anailipa Halmashauri fedha kiduchu ni mtumishi wa Serikali jina linahifadhiwa ,Alisema Bw.Msema. 

Kwa masikitiko makubwa Bw.Msemwa ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Soko kuu Mafinga alisema unyonyaji na ufisadi unaofanywa na Wajenzi wa vibanda vipya hausemwi ila Wajenzi wa vibanda vya zamani ndio wanao onekaana wamekaa muda mrefu huku wakiinyonya Serikali.                                                

" Mfano Mimi Kodi ya mapato kwa mwaka makadilio yangu ni kati ya sh.350,000 hadi 450,000 kwa mwaka lakini kwa hesabu za Mkuu wa Wilaya na Mkuu wa Mkoa wanalazimisha nilipe sh. 960,000 kwa mwaka " Alisema Damiani Kyando 

Bw.Kyando alisema kwanini Mkuu wa Wilaya na Mkuu wa Mkoa wameshindwa kukaa na Wafanyabiashara ili waweze kuwasikiliza badala ya kuwa wanafika na kupanga bei zao ? Ili hali Mkurugenzi na Baraza la madiwani wapo ? Alihoji.                    

Alimaliza kusema biashara sio ugomvi wala vita Polisi,Wanajeshi na Uhamiaji wanini kama Kodi inalipika na ni rafiki?                      Utawala bora uendane na vitendo na sio nguvu na vitisho" Alisema Bw.Kyando.





 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI