NA AMON MTEGA
RUVUMA
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan amesema atakuwepo ziara Mkoani Ruvuma kwa takiribani siku nne kukagua miradi mbalimbali pamoja na kuizindua miradi iliyokamilika .
Hayo amesema wakati akiwahutubia maelfu ya wakazi wa Manispaa ya Songea Mkoani humo alipokuwa akifunga Tamasha la tatu Taifa la Utamaduni ambalo limefanyika Mkoani Ruvuma .
Rais Dkt Samia Suluhu Hassan amesema kuwa katika Mkoa wa Ruvuma zimeletwa fedha nyingi za miradi mbalimbali hivyo nilazima kuipita kuangalia utekelezaji wake
Amesema kuwa wakati akiwasili Mkoani humo ametembelea ujenzi wa Ujenzi wa Uwanja wa Ndege uliyopo kata ya Luhuwiko Manispaa ya Songea huku akisema amefurahishwa na ujenzi jambo ambalo litafanya Mkoa huo kuwa wakibiashara kwa kuwa kutakuwa na ongezeko la wageni wengi.
Aidha katika hatua nyingine wakati akifunga Tamasha hilo ameipongeza wizara ya Utamaduni,Sanaa na Michezo kwa kuandaa Tamasha hilo huku akiitaka Wizara hiyo kuendelea kusimamia maadili kwenye jamii ili kulinda Utamaduni wetu .
Kwa upande wake Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt Damas Ndumbaro amesema Tamasha hilo litakuwa linafanyika kwa mikoa yote kwa awamu na sasa ulikuwa mkoa wa Ruvuma .
Mwisho .
0 Comments