Header Ads Widget

PWANI KUSHIRIKIANA NA WAWEKEZAJI SEKTA YA ELIMU.

 


MKOA wa Pwani umesema utaendelea kuunga mkono uwekezaji wa elimu unaofanywa na sekta binafsi kwani unaisaidia serikali kuinua kiwango cha elimu.


Hayo yamesemwa mjini Kibaha na Katibu Tawala wa Mkoa huo Rashid Mchatta  wakati wa mahafali ya Shule za Kibaha Independence School (KIPS) Main, Annex na Msangani.



Mchatta amesema serikali inashirikiana na sekta binafsi kwenye uwekezaji huo kwa usimamizi na uboreshaji wa miundombinu ili elimu itolewe kwenye ubora.


Awali akimkaribisha mgeni rasmi mkurugenzi wa kampuni ya Njuweni Ltd Yusuph Mfinanga amesema wazazi wanapaswa kutenga bajeti kwa ajili ya kusomesha watoto.



Kwa upande wake kaimu ofisa elimu Halmashauri ya mji Kibaha Adrian Livamba amewataka wamiliki shule binafsi kuhakikisha shule hizo zinazingatia vigezo na ubora wa walimu.


Naye Mwalimu mkuu wa KIPS Msangani Ramadhan Hussein ametaja baadhi ya changamoto za shule kuwa ni ubovu wa barabara.



Mwakilishi wa wazazi Emanuel Kulaya amesema kuwa wanafunzi hao wamelelewa kwenye mazingira mazuri na nidhamu ya hali ya juu.


Jumla ya wanafunzi 154 kutoka shule hizo walitunukiwa vyeti vya kuhitimu elimu ya msingi.


Mwisho

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI