Na Shemsa Mussa -Matukio daima App
Kagera.
Walimu na Wakuu wa shule za Msingi katika Mkoa Kagera wamepewa Mafunzo ya uongozi na usimamizi fanisi wa shule ikiwa ni njia Moja wapo ya kuwakumbusha kufanya kazi kama walezi na kwa mujibu wa Sheria.
Akizungumza katika Mafunzo hayo yaliyofanyika katika shule ya sekondari kashozi iliyopo Ndani ya Halmashauri ya Bukoba Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu (ADEM) Dkt Maulid J Maulid amesema lengo la Mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo kwa kuongeza maarifa na namna nzuri ya kuwa kiongozi Bora kwa walimu na wadau wa Elimu kwa ujumla.
Pia amasema,ili kukamilisha maendeleo ya elimu lazima kuwepo uongozi imara na kusema kuwa kutokuwepo kwa uongozi Bora katika shule hakuna dira yoyote nzuri inaweza kutekelezwa hivyo ni jukumu la Wakuu wa shule kujitambua na kujua namna wanavyoiongoza taasisi kubwa ya Elimu.
"Tunafahamu taasisi ya shule sio tu Mkuu wa shule na walimu bali taasisi ya shule ina wanafunzi,walimu,wazazi,jamii inayoizunguka shule na wadau wengine wa Elimu kuanzia wizara mpaka ngazi ya Kijiji na sifa ya kuwa Mkuu wa shule au taasisi ni kuhakikisha una maarifa na vigezo vinavyohitajika ili uweze kuongoza taasisi ambayo ni shule, amesema Dkt Maulid"
Dkt Maulid amewasisitiza walimu kuwa na maono pamoja na shule kwa ujumla na kusema kuwa mipango ya maendeleo ya shule lazima ihakisi mabadiliko katika sera na Mitaara ya elimu hivyo inapotengenezwa mipango ya madabiliko ya shule lazima ihakisi mabadiliko yanayoendelea ndani ya wizara ya elimu na Taifa kwa ujumla.
Aidha Dkt Maulid amewataka walimu kuwa wabunifu na kusimamia maadili na Uzalendo kupitia uongozi walionao wa Ukuu wa shule na kuziheshimu na kuzipatia nafasi jumuhiya za wazazi ili ziweze kutoa masaada kwa kamati za shule na uongozi wa shule ili kushirikiana kwa pamoja na kuleta mikakati ya ufahuru mzuri kwa wanafunzi,na kuishi kwa kupeana taarifa kubadilishana uzoefu kwa kushauriana ili kuepuka migogoro.
Nae Mgeni rasmi katika Mafunzo hayo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Bukoba Bi Fatina Hussein Laay ametoa shukrani kwa wasimamizi wa Mafunzo hayo kwa kuuona Mkoa Kagera na hasa Halmashauri hiyo na kuwapongeza walimu kujitokeza kwa wingi, pia amesisitiza walimu kuchangamka hasa jinsia ya kiume kujipenda na kuyapenda mazingira ya shule kwa kuyaweka katika muonekano mzuri wa usafi zaidi.
"Najua wanaume walio wengi hatujipendi na tuna mambo mengi Si ndio ila tukishakuwa kiongozi au Mkuu wa shule lazima ubadilike jamani,nilipita kwenye shule kabla ya Mitihani ya darasa la Saba ili nilipokuwa naenda kwenye shule inayosimamiwa na Mkuu wa shule Mwanamke unakuta inang'aa sana mazingira yanapendeza ,ila kwetu sisi wanaume Mmmmh,inabidi tubadilike,amesema Bi Fatina "
Pia naye Mratibu wa Mafunzo Bw Venant Fundi amesema jumla ya walimu 142 wameweza kushiriki Mafunzo hayo na 114 kati yao ni jinsia ya kiume sawa na asilimia 80.3 na 28 ni jinsia ya kike sawa na asilimia 19.7 na kusema Mafunzo hayo yatafanyika ndani ya siku tatu .
Hata hivyo nao washiriki wa Mafunzo hayo Mwl Methodius Majojo M/M katika shule ya Msingi Magonge na Mwl Hassan Masoud M/M shule ya Msingi kansenene kwa ujumla wao wameushukuru Miradi wa Boost na Word Bank kwa kuwapatia Mafunzo ya kuwanoa na kuwajengea uwezo kwa kuwakumbusha mambo mengi ikiwemo Uongozi usimamizi na utawala wa shule pamoja na usimamizi wa miundombinu ya shule ,ufundishaji na ujifunzaji ufanisi shuleni.
0 Comments