Na MWANDISHI WETU
MAKAMU Mwenyekiti wa Act Wazalendo Taifa Ismail Jussa Ladu amesema iwapo chama cha Act kitashika mwaka 2025 katika kipindi cha miaka mitano ajira zitawatafuta vijana badala ya vijana kutafuta ajira visiwani Zanzibar.
Makamu mwenyekiti Jussa ameyasema hayo wakati akihutubia maelfu ya Wananchama wa chama hicho katika mkutano wa hadhra uliofanyika katika uwanja wa Mpira wa konde Polisi, Jimbo la Konge Wilaya ya Mcheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba.
Alisema tatizo la ajira hivi sasa Zanzibar ni kubwa na linawapa wakati mgumu wazazi baada ya kusomesha Watoto wao kwa mikopo lakini baada ya kuhitimu wamebakiwa nav yeti huku ajira zikiwa hazionekani.
“Vijana wengi wanakabiliwa na tatizo la ajira na wazazi wao wanawasomesha kwa mikopo lakini wamebakiwa na madeni huku Watoto wao wakiwa na vyeti vya kuhitimu bila ya kuajiriwa, walioahidi ajira laki Tatu zipo wapi,”
Aidha alisema kisiwa cha Pemba kinakabiliwa na tatizo la mfumuko mkubwa wa bei ikiwemo bei ya Mchele aina ya mapembe ambao umefikia kilo moja Shilingi 24000 na kuwapa wakati mgumu wananchi wa chini.
Alisema Pemba haiwezi kufunguka kiuchumi bila ya kuwa na bandari ya kisasa na uwanja wa ndege wa kimataifa ili bidhaa ziweze kuingia moja kwa moja badala ya kusafirishwa mara mbili kutoka Nje ya nchi na kupitia katika bandari ya Malindi Unguja.
Alisema Serikali ya awamu ya nane imekiri hadharani kuwa Zanzibar ina kiwango kikubwa cha umasikini wa maihitaji ya watu, ukosefu wa ajira,udumavu wa Watoto kwa asilimia 30 kutokana na lishe duni pamoja na ukosefu wa ukuwaji wa teknolojia.
“Hayo sikusema mimi Jussa kasema makamu wa pili wa Rais Hemdi Suleiman Abdulla huko Tunguu Agost 31 wakati akizindua Dira ya mpanago wa maendeleo ya Taifa 2025,”
Nae Mwenyekiti wa Chama hicho Taifa, Othman Masoud Othman amesema Wilaya ya Micheweni pamoja na kuwa utajiri mkubwa wa ardhi na rasilimali za baharini lakini ndio Wilaya inayoongoza kwa umasikini na utapia mlo kwa Watoto wakati ina kilomita za mraba 231 sawa na Mkoa wa Mjini Magharib Unguja.
Alisema Wilaya ya Micheweni ni eneo moja lipo karibu na Mombasa Kenya na mwambao wa Tanga Tanzania bara lakini limeshindwa kuwa kituo cha biashara kutokana na kukosekana na miondombinu ya uhakika ya usafiri na uchukuzi.
“Miaka ya nyuma mwalimu alikuwa anaheshimika sana lakini sasa ili kujiongezea kipato mwalimu anaendesha bodaboda na askari mwenye cheo cha kamshna Msaidizi wa Polisi akistafu anakuwa kondakta wa Daladala na kama alinunua gari kwa mafao aikichakaa anauza chuma chakavu,”
Kwa upande wake Naibu katibu Mkuu wa chama hicho Omar Ali Shehe amewatahadharisha vijana kuwa makini na maneno ya propaganda kuelekea uchaguzi Mkuu mwaka 2025 kuwa watapewa ajira wakati wanaotoa ahadi hizo Watoto wao hawana ajira.
Joto la kisiasa limeanza kujitokeza mapema kati ya chama cha Act Wazalendo na CCM kila mmoja akimshutumu mwenzake wakati chama tawala kinasema miaka Minne ya Uongozi wa Rais Dkt Hussein Ali Mwinyi kumepatikana maendeleo makubwa ambayo hajawahi kutokea wakati upinzani wakidai umasikini na ufisadi umeongezeka.
0 Comments