NA HADIJA OMARY LINDI......
CPA Hosseah Hopaje Lugano amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa Chama cha soka Mkoa wa Lindi(LIREFA)kwa miaka minne tena kupitia uchaguzi uliofanyika Leo Sept 24 katika ukumbi wa Sea view beach resort manispaa ya Lindi.
Mwenyekiti wa chama cha mpira wa miguu MKoa wa Lindi CAP Hosseah Lugano ametetea nafasi yake ya uongozi kwa mara ya pili baada ya kushinda kwa kura za ndio katika uchaguzi mkuu uliofanywa na chama hicho huko Mkoani Lindi
Uchaguzi huo ulioendeshwa na kamati ya uchaguzi na kusimamiwa na TFF ulihusisha pia nafasi za wajumbe wa mkutano Mkuu Reule Nyaulawa, kamati ya utendaji ambao ni Abdala Kipingo na Sande kachele, huku Mwenyekiti huku mwenyekiti akiwapendezeka Ally selemani MKadeba,Juma Nandonde,Sharifa mkwango kuwa wajumbe na Ahmed Bongi kuwa Makamu mwenyekiti .
Awali akufungua Mkutano mkuu wa kawaida wa chama hicho Afisa Elimu wa Mkoa wa Lindi Joseph Mabeyo kwa niaba ya katibu tawala wa mkoa wa Lindi amewataka viongozi watakaochaguliwa kuimarisha msingi wa mpira wa miguu kwa kuwekeza Katika soka la vijana .
Amesema Mpira wa miguu si tu mchezo bali ni chombo cha kujenga umoja, furaha, na maendeleo ya jamii hivyo Kama viongozi wa michezo wanatakiwa kuimarisha msingi wa mpira wa miguu kwa kuwekeza katika soka la vijana kwa kuwapa fursa vijana ya kuonyesha vipaji vyao ili waweze kuzifikia ndoto zao.
Mwenyekiti wa LIREFA Hosseah Hopaje Lugano pamoja na kuwashukuru kwa kumchagua kushika nafasi hiyo kwa mara nyingine pia ameahidi kutimiza azma ya kuwa na mfumo wa mashindano bora Katika mkoa huo wa Lindi , kwa kufuata maelekezo na kanuni za mashindano zilizotolewa na TFF.
Alisema mkakati wao kwa sasa ni kutilia mkazo maendeleo ya soka la vijana,Beach soccer na mpira wa miguu wanawake pamoja na eneo la mafunzo ya taaluma za soka kwa makocha na waamuzi, michezo mashuleni na kuhamasisha ujenzi wa vituo vya kukuzia vipaji vya vijana.
Alieleza mkakati mwingine ni ujenzi wa viwanja vya mpira wa miguu, kupambana na matumizi ya madawa ya kulevya/kuongeza nguvu na vitendo vyote visivyofaa katika mpira wa miguu Katika Mkoa na taifa kwa ujumla.
Baadhi ya wajumbe wa mkutano huo wakaeleza matarajio Yao kwa viongozi waliochaguliwa Katika kuendeleza soka la Mkoa huo
0 Comments