Header Ads Widget

HAYA NDIYO YANAYOSADIFU SIFA YA 'DODOMA FAHARI YA WATANZΑΝΙΑ'


NA AUGUSTA NJOJI, DODOMA

SHUGHULI za serikali kuhamishiwa Dodoma, ni miongoni mwa sifa zinazo fanya mkoa huo kuwa "fahari ya watan zania.

Ni uamuzi unaotajwa kuchochea zai di kukua kwa kasi mkoa huo kutokana na uwekezaji mkubwa unaofanywa na serikali, hasa kwenye huduma na mi- undombinu ili kusadifu sifa na hadhi ya Makao Makuu.


Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule, anasema Dodoma ni eneo la kimkakati na linafikika kwa ura- hisi kwa watanzania wanaotoka pande cote za nchi na ndio sababu ya kuwa ahari ya watanzania.

Anasema tangu serikali kuanza ekelezaji shughuli zake mwaka 2017, endeleo yamekua kwa kasi zaidi nganishwa na kipindi kingine cha na na viongozi wanatamani kuona

mkoa huo kwa sura yenye hadhi ya wa tanzania.

"Kwa sasa Dodoma kuna ongezeko kubwa la watu, si watumishi tena, wengi wanaokuja ni sekta binafsi ambao ni wa- fanyabiashara, ofisi za kijamii zinakuja kwa sababu wanasema 'wateja wetu na watu wa kufanya nao kazi wako Dodo ma'," anasema.

Anasema kuwa kutokana na ongeze ko hilo, serikali imefanya kazi kubwa ya ujenzi wa miundombinu ya kuwezesha wananchi kupata huduma zinazostahili na zenye hadhi ya Makao Makuu.

"Tumeshuhudia miundombinu am- bayo haijazoeleka kwa mikoa mingine, mfano barabara ya mzunguko. Hii yote ni kufanya Dodoma kuwa mkoa wa ki pekee usio na msongamano katikati ya mji na usio na mwingiliano wa magari," anasema.

Mkuu wa Mkoa anasema uwekezaji wa miundombinu na kuanza kwa safari

za treni ya mwendokasi (SGR) Dodoma hadi Dar es Salaam ni fahari kwa wa-

nanchi na wafanyabiashara nchini. "Kwa sasa watu wanatoka Dar es Sa laam kuja Dodoma kufuata huduma kwenye wizara. Kuna wafanyabiashara wanatoka hapa asubuhi wanakwenda Kariakoo, wananunua bidhaa wanarudi lakini wengine wanakuja na treni ya jioni ili waondoke na magari ya usiku kwenda mikoa mingine, hii ndo fahari

ya watanzania. "Mji wa Serikali Mtumba unaendelea kukamilika sasa hivi wizara tatu zime-

shahamia kwenye majengo yao, majen go mengine yanaendelea kukamilika na inatarajiwa Desemba mwaka huu mengi yawe yamekamilika na itawezesha wa- nanchi kupata huduma sehemu moja

hasa huduma za wizara," anasema. Anasema Dodoma inatarajia kuwa na uwanja wa ndege wa kimataifa unao- Jengwa eneo la Msalato na tayari Rais

ametoa takribani Sh. bilioni 365 kwa ajili ya kujenga uwanja huo wa kisasa wenye njia ndefu ya kuruka na kutua ndege to- fauti na viwanja vingine.

MIKAKATI KIUCHUMI

Mkuu wa Mkoa anasema kuwa mwa- ka jana walifanya utafiti kwa kushiriki- ana na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) ili kujua kipato cha mwananchi na mkoa huo na waliona kipato kipo chini ya ki- wango cha kitaifa.

"Baada ya utafiti tulikuja na maeneo manne yatakayonyanyua kipato cha

mkoa na mwananchi maana utafiti ulitu- saidia sana ulionesha maeneo yatakayo- saidia, wananchi wa Dodoma asilimia 72 wanategemea kilimo. Nimshukuru Rais Samia Suluhu Hassan amebadili mtaza- mo wa Dodoma kwenye suala la kilimo na imani ya kuwa Dodoma ni kame," anasema.

uvunaji maji ya mvua kwa kujenga ma bwawa makubwa ambayo yanakuwa na miundombinu ya umwagiliaji ili wananchi walime mwaka mzima kwa kumwagilia


"Na sisi tumepanga Dodoma kuwa gha la la Tanzania la chakula, tumepata bahati ya kuwa na mabwawa makubwa na ujenzi wa mabwawa matano, upo katika hatua mbalimbali, anasema.


Anabainisha kuwa mkoa umepokea zaidi ya Sh. bilioni 114 kwa ajili ya miradi ya umwagiliaji ambapo kwa wilaya ya Mp wapwa linajengwa bwawa lenye uwezo wa kumwagilia ekari 20,000, wilaya ya Chamwino eneo la Ndogoe kuna bwawa linajengwa lenye uwezo wa kumwagilia ekari 11,000, eneo la Membe ekari 8,000,


Chinangali ekari 17,000, Anasema kuwa mwaka wa fedha 2024/25 wana miradi sita mikubwa ina tarajiwa kutekelezwa na itatatua tatizo la mafuriko.


Anasema Uwanja wa Nanenane, Nzu guni utakuwa wa kimataifa wa maonesho ya kilimo na ndani yake kuna kiwanda cha kuunganisha matrekta.

"Kupitia Jiji tumesema haya mazao ya mboga tunataka kuwe na kiwanda kikub wa cha kuchambua na kufungasha kusa firisha kwenda nje ya nchi.

"Tutahamasisha wananchi walime kupitia miundombinu ya umwagiliaji iliyowekwa na kusafirisha kupitia SGR. tumeambiwa kuna mabehewa ya kusafiri sha, anasema.

Kuhusu zabibu, Mkuu wa Mkoa anase- ma wameamua kulipa zao hilo uzito wa kipekee kama zao la kiuchumi na litapam banua Dodoma kama zao la kiuchumi na

kiutalii.

"Tutakuwa na mashamba ya zabibu ya taendelezwa na kulimwa kisasa, tunataka zabibu iwe zao la kimkakati kutokana na kuwa na upekee wa kuvunwa mara mbili kwa mwaka tofauti na nchi zingine duni ani," anasema.

UTALII

Mkuu wa Mkoa anasema kipaumbele kingine ni kujiimarisha kwenye utalii kwa kuwa Dodoma kuna kila kitu kinachopas wa kubadilishwa kuwa utalii.

"Tuna utalii wa zabibu, ngoma za utamaduni tukiweka utaratibu watu wa mataifa mengi watakuja Dodoma, kuna mapori yana wanyama wa aina zote. Kuna eneo la wapigania uhuru Kongwa litaanza kuboreshwa, historia iliyopo pale inaone sha Tanzania ilivyo na thamani kubwa kwenye ukombozi bara la Afrika, anasema

Anasema kuna mwekezaji ameanza kuwekeza hoteli ya nyota tano kwenye pori la Mkungunero, kuna michoro ya ki historia ya Kolo ambayo haipatikani eneo lingine zaidi ya Kondoa.

"Tumejipanga kuifungua Dodoma kupitia utalii kwa sababu ni 'connection' ya utalii kwenda Hifadhi za Taifa Ruaha. Tarangire, Mikumi na Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro (NCAA).

Tunataka Dodoma iwe inafanyika mi kutano ya kimataifa, hivyo kuna fursa ya utalii wa mikutano, tunaendelea kuimari sha miundombinu," anasema.

Anaongeza kuwa wamejipanga kuwapo utalii wa michezo na kwamba inahitajika kuwapo hoteli za nyota tano zisizopurigua tano, viwanja vya mazoezi vitano na wako

tayari kupokea mashindano ya soka ya da Mataifa ya Afrika (AFCON).

UWEKEZAJI

Mkuu wa Mkoa anasema wana mkakati wa kuifanya Dodoma kuwa kituo cha us ambazaji wa vitu maeneo ya ndani na nje ya nchi kutokana na kuwa na miundom binu muhimu ya usafirishaji. "Inajengwa bandari-kavu ambayo tu

natarajia kabla ya Desemba mwaka huu itaanza kufanya kazi, Mamlaka ya Bandari (TPA) wanashirikiana na wadau wa sekta binafsi na wengine wameshapewa mae neo thumwa, inapejengwa bandari kavu," anasema

Mkuu wa Mkoa anasema kuwa mwaka huu wanatarajia kuanza mchakato wa kujenga soko la kimataifa la bidhaa mbal imbali kama Kariakoo ili mikoa kama Kagera, Mwanza, Tabora, Simiyu, Singida, Shinyanga na Katavi wapate bidhaa kwa urahisi badala ya kwenda Dar es Salaam.

"Nia ya serikali ni kutengeneza mazin gira mazuri kwa wananchi wafanye shu ghuli zitakazowawezesha kujikwamua kiuchumi, anasema.

VIWANDA

Mkuu wa Mkoa anasema kipaumbele kingine cha kiuchumi ni viwanda kuto- kana na kuwa na malighafi za kilimo na

madini. "Kuna viwanda vimeanzishwa karna kile cha kuunganisha matrekta, kipaumbele

chetu ni viwanda, kuna maeneo yamet- enga kwa ajili hii. Kwa Jiji la Dodoma kuna eneo la Nala viwanda vikubwa, Msalato viwanda vya kati na wilaya zingine zote za Dodoma maeneo yametengwa ya viwana nasema.

MADINI

Mkuu wa Mkoa anasema Dodoma ina aina nyingi za madini ambayo ni ya kim- kakati na tangu itangazwe taarifa ya GST mwaka jana, kumekuwapo mwamko mkubwa wa wawekezaji, ikiwamo kam- puni ya GGM ambayo inakamilisha taarifa

yake ya utafiti eneo la Chemba. "Kule Mpwapwa kuna madini ya shaba

ambapo kuna wawekezaji wakubwa kuto- ka Marekani wameonesha nia," anasema.

WAWEKEZAJI WAITWA

Mkuu wa Mkoa anasema kuna mahi taji ya hoteli za nyota tano ambapo tatu zinatarajiwa kukamilika hivi karibuni ili kuchangamkia mahitaji ya mashindano ya AFCON.

"Utalii unahitaji hizi hoteli, mikutano na michezo, hivyo hii ni fursa ya uwekezaji wa ndani na nje, tunahitaji kumbi za kisasa za kimataifa zijengwe, tunahitaji wawekezaji fursa za madini, tunahitaji wawekezaji kwenye kilimo, viwanda hizi ni fursa, mji wa kimkakati wa 'logistic ni fursa, yaani ukiona Dodoma tu ni fursa. anasema

Anasema mkoa uko tayari kuwapokea wawekezaji na mazingira mazuri ya mewekwa ikiwamo upatikanaji huduma muhimu za kijamii.

HUDUMA ZA KIJAMII

Mkuu wa Mkoa anasema kuna upati kanaji shule na hospitali bora ikiwamo ya Benjamin Mkapa ambayo inatoa huduma za kibingwa na kuwa kimbilio la wananchi wa ndani na nje ya nchi.

#Nchanzo :Nipashe


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI