Kiwanda kikubwa kinachojengwa Mkoani Dodoma kitapelekea ongezeko la upatikanaji wa mafuta ya kupikia nchini.
Kiwanda hicho kinachojengwa eneo la Veyula kina uwezo wa kuchakata tani 250 za alizeti kwa siku.
"Ma afisa kilimo hakikisheni mnaongeza uzalishaji wa alizeti kutumia kilimo cha umwagiliaji ambao Mh. Rais Samia ametujengea mabwawa makubwa ili tulime mara mbili kwa mwaka. Hamasisheni wakulima kwani kuna uhakika wa soko" . Alisema Senyamule - RC Dodoma.
Kiwanda hicho kinamilikiwa na kampuni ya Mainland Africa ni mkombozi mkubwa kwa wakulima wa zao la Alizeti Dodoma .
0 Comments