Header Ads Widget

DKT.BITEKO AMEZITAKA MAMLAKA ZA UNUNUZI WA EAC KUHAKIKISHA YANASIMAMIA MALENGO YALIYO KUSUDIWA

 




Na,Jusline Marco;Arusha

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Madini Dkt.Dotto Biteko amesema serikali imeendelea kudhibiti matumizi ya fedha zinazopelekwa kwenye kila fungu kwa kutumia njia mbalimbali ikiwemo mifumo ya Kieletroniki ili kuleta tija na ufanisi unaostahili kwenye utekelezaji wa bajeti ya fungu husika.



Akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan katika Ufunguzi wa Jukwaa la 16 la Ununuzi la Umma la Afrika Mashariki na Uzinduzi wa Mfumo wa Kieletroniki wa ununuzi wa umma NEST, Dkt.Biteko amesema kutokana na changamoto za kimifumo serikali kupitia wizara ya fedha iliamua kujenga mfumo mpya kieletroniki wa ununuzi wa umma NEST.



Aidha aliongeza kwa kutoa wito kwa mamlaka zote za ùnunuzi wa umma kutoka nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kuhakikisha wanasimamia malengo waliyojiwekea ili tija na ufanisi uweze kupatikana katika usimamizi wa sekta ya manunuzi ili huduma kwa wananchi iendelee kupatikana kwa wakati na kwa ufanisi.



Dkt.Biteko alisema serikali imekuwa makini kuhakikisha fedha zinazotumika kupitia ununuzi wa umma zinapata usimamizi makini na kuipa wizara ya fedha jukumu la kuhakikisha linaandaa sera ya Taifa ya mkakati wa usimamizi wa mnyororo wa ugavi ili kuhakikisha ununuzi na shughuli zote zinazofunganishwa katika mnyororo huo zinazofanyika kwenye taasisi za umma zinazozingatia sera hiyo na mikakati  waliyojiwekea.



Naye Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Natu El Maamry Mwamba amesema kuwa Jukwaa hilo limelenga kuwakutanisha wadau kuzungumzia masuala ya ununuzi wa umma kwa  manufaa ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.



Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Ununuzi wa Umma PPRA, Dkt. Leonada Mwagike ameipongeza Serikali kwa kufanya maboresho makubwa katika sekta ya ununuzi wa umma na kuleta tija ya kuongeza uwajibikaji ili kupata thamani halisi ya fedha inayoonekana na kusema kuwa Mfumo huo unasomana na taasisi 17 ya mifumo ya Serikali.



Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti ya Ununuzi wa Umma PPRA, Bw. Dennis Simba amesema kuwa majukwaa hayo hukutana kupitia nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ambapo huwa na majadiliano na maazimio na katika Jukwaa la 16 washiriki watapata fursa ya kuangalia utekelezaji wa maazimio ya jukwaa la 15.



Sambamba na hayo Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Serikali Mtandao, Mhandisi Benedict Ndomba amesema ili kuwa na seriÄ·ali mtandao madhubuti,upatikanaji taarifa kidigitali ni kiungo muhimu ambapo ametaja moja ya jukumu la taasisi hiyo kuwa ni pamoja na kusimamia matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano kwa umma na inatambua kuwa ununuzi wa umma nchini ni eneo linalohitaji kusimamiwa vizuri ili kuleta matokeo tarajiwa.



Awali akitoa neno la ukaribisho Mkuu wa Wilaya ya Monduli Festo Kiswaga akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha Paul Makonda amewataka wafanyabiashara kuwekeza katika fursa za utalii sambamba na kuchanhamkia zabuni ambazo zinatangazwa ndani na nje ya mkoa kipitia mfumo wa nest.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI