Header Ads Widget

WAZAZI MUFINDI KATAEENI , KEMEENI MIMBA KWA WANAFUNZI.

 


Na Fredrick Siwale -Matukio Daima APP Mufindi.


WAZAZI Mufindi kataeni Mimba kwa Wanafunzi Mashuleni na toeni taarifa badala ya ninyi kuwa sehemu ya kuficha watenda uovu kwa Wanafunzi,


Rai hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Viwanda na Mbunge wa Jimbo la Mufindi Kaskazini Exaud Kigahe aliyekuwa mgeni rasmi Katika mkutano wa Baraza la Wazazi Wilaya ya Mufindi .


Kigahe alisema ni wakati sahihi kwa Wazazi na Wananchi kusimama kidete kukemea kwa nguvu moja ili kusomesha tabia ya utoro na Mimba kwa Wanafunzi wa Shule za msingi na Sekondari.


"Ndugu zangu Serikali inatoa fedha nyingi sana za Miradi ya Maendeleo ikiwepo hii ya elimu lengo likiwa ni Watoto wasome na siku za mbeleni waje kuwa Viongozi halafu mnataka turuhu Shule kuwa Viwanda vya kuzalisha Watoto kwa Mimba za utotoni haikubariki! " Alisema Kigahe.



 Upande wake katibu wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Iringa Hamza Adam Kyeibanja amekemea Mimba kwa Wanafunzi katika Shule za msingi na Sekondari,ikiwa ni pamoja na kuwataka Wazazi na Wananchi kutoa taarifa kwenye vyombo vya dora na Mamlaka za Serikali ili kukomesha tabia hizo za hivyo.


Kyeibanja akiwa amechukizwa na Matukio hayo kwenye kikao cha Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Mufindi,ambacho kimefanyika katika Ukumbi wa Bomani Wilaya ya Mufindi aliwataka Wazazi kusimama kwa miguu yao wenyewe kuwalinda Watoto wao.


Kyeibanja alisema kama Mtendaji Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Iringa amesikiliza hoja za Wajumbe wakilalamikia Mamlaka za Serikali kuwa hawachukui hatua kudhibiti Matukio ya Wanafunzi kupewa Mimba na Watu wasiojulikana na wakati mwingine Wanafunzi kutoroshwa kwa madai ya kuwa hawajulikani waliko torokea alisema haiingii akilini .                


Kyeibanja alisema malalamiko ya Walimu kuzuiwa kuwapeleka Watoto wao Vituo vya afya kupima ujauzito , alisema Wizara ilitoa Waraka na jukumu hilo kuachiwa Wazazi .


" Haiwezekani eti kwenye  tawi na Kata Kuna Viongozi wa Jumuiya ya Wazazi halafu eti Kitogojini, Kata  au katika Mtaa kuna mwanafunzi haonekani kisa amepewa Mimba halafu Kiongozi upo fahamu hufai kuendelea kuwa Kiongozi."Alisema Kyeibanja.


Hivyo amewataka Viongozi na Wananchi ambao ndio Wazazi kushirikiana kufichua vitendo vya uhalifu na ukatili wa kijinsia kwani wanaishi na baadhi yao.     


Alisema kama Jumuiya ya Wazazi Mkoa halitakuwa tayari kuona vitendo hivi vinaendelea halafu lawama watupiwe Walimu au Mamlaka za Serikali.


"Narudi Iringa mjini ninakwenda kuwachongea kwa kushimdwa kuthibiti vitendo vya Ukatili wa kijinsia na Mimba mashuleni Ili hali Wahusika mnaishi nao ,toeni Ushirikiano kwenye Mamlaka na kemeeni kutoka Moyoni na sio kuleana na kufichiana siri na wanao tuharibia Watoto wetu" Alifoka kwa hasira.


Upande wake Mjumbe wa Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Mufindi Gabriel Mahenge aliomba Serikali irudishe Usimamizi na ufuatiliaji wa Maadili kwa Walimu ili kusimamia mienendo na tabia za Wanafunzi badala  ya kuachiwa Wazazi peke yao.


Gabriel alisema kwa pamoja Walimu, Wazazi na Jamii wakishirikiana ,upo wezekano wa kuthibiti Mimba na utoro mashuleni ikiwa ni pamoja na vikao vya mara kwa mara na elimu juu ya malezi na Maadili.         

............ Mwisho............

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI