Header Ads Widget

WAWEKEZAJI WALIOSAJILI MIRADI YAO TIC KUNUFAIKA NA VIVUTIO VYA KODI




Meneja wa Uhamasishaji uwekezaji wa ndani kutoka kituo cha uwekezaji Tanzania (TIC ), Ndugu Felix John ameeleza kuwa wawekezaji wa ndani ambao wamejisali miradi yao kupitia TIC wananufaika kupitia vivutio vya kikodi na vivutio visivyo vya kikodi . Vivutio vya kikodi pamoja na msamaha wa kikodi wa ushuru wa forodha wa vifaa mbalimbali vinavyoagizwa nje ya nchi kwaajili ya uwekezaji .


" Kituo cha uwekezaji Tanzania (TIC) kimsingi ni wawezeshaji ambao tunawawezesha wawekezaji kuweza kufikia azma zao na ndoto zao za kuwekeza katika nchi yetu ili Taifa liweze kunufaika  na uwekezaji wao " Felix John .


Felix ameyaeleza hayo alipokuwa anazungumza na waandishi wa habari akiwa katika eneo la uwekezaji wa mkodi  ambao unaitwa Sheby Investiment Limited uliopo Nondwa wilaya ya Kilwa Mkoani Lindi .



Aidha, ametumia fursa hiyo kueleza dhamira ya TIC kutembelea Mkoa wa Lindi ni kuhamasisha wawekezaji wa ndani kuwekeza ndani ya nchi yao, hiyo ni dhamira ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM). 



Hamasa hiyo inawalenga wawekezaji wa ndani , waandishi wa habari na wafanyabishara ambapo watapata elimu ya umuhimu wa kuwekeza ndani ya nchi yao.


TIC wametembea uwekezaji wa Hotel ambayo ni Sea View Lindi Resort ambayo imetumia Bil 2.4 kuwekeza na Mgodi wa Sheby Investment Limeted ambao unazalisha zaidi ya Tani 800 hadi 900 kwa siku.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI