Header Ads Widget

TAKUKURU YABEBESHWA RUNGU LA KUCHUNGUZA MIKOPO YA HALMASHAURI SAME.

 


NA WILLIUM PAUL, SAME. 



MKUU wa wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro, Kasilda Mgeni ameigiza Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) Wilaya humo kuchunguza vikundi vilivyokopeshwa fedha za mikopo inayotolewa na Halmashauri kwa makundi ya Wanawake, Vijana na Walemavu kubaini kama fedha hizo zilitolewa kwa walengwa lakini pia changamoto zinazofanya baadhi yao kushindwa kurejesha kwa wakati.



Kasilda ametoa agizo hilo wakati akizungumza na baadhi ya wanachama wa vikundi ambavyo mpaka sasa vinadaiwa marejesho na Halmashauri ambapo amesisitiza kua wanaokopa fedha hizo warudishe kwa wakati ili ziweze kuwa na matumizi endelevu.



Aidha amewatahadharisha watumishi wa Umma na Madiwani kujiepusha na fedha hizo huku akisema wanapaswa kutambua kuwa lengo la kutolewa kwa fedha hizo ni kuwawezesha wananchi wa kawaida ili waweze kujikwamua kiuchumi na si watumishi wa Umma wala Madiwani.



Mwisho.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI