Mashirika yasiyo ya kiserikali Mkoani Lindi yamehaswa kushirikiana kwa pamoja Katika kufikisha ujumbe kwa Jamii juu ya Umuhimu wa kuwekeza Katika malezi makuzi na maendeleo ya watoto.
Wito huo umetolewa na Mjumbe wa kamati ya uhamasishaji wa mpango wa Taifa PJT-MMMAM Mkoa wa Lindi kutoka Shirika la utetezi wa Wanawake Lindi Bwa. Nelson Choaji alipokuwa akielezea utekelezaji wa program hiyo wakati wa kikao kazi kilichowakutanisha wajumbe wa kamati ya Nacongo
Kamati hiyo inahusisha wasajili wasaidizi, waratibu wa NGO's pamoja na Wawakilishi wa Baraza la Taifa la Mashirika yasiyo ya Serikali Ngazi za Wilaya
Nelson Amesema ili program hiyo iwafikie wananchi wengi zaidi ni muhimu kushirikiana kwa pamoja baina ya Serikali pamoja na Wadau wengine kwa kupenyesha Ajenda za maswala ya malezi Katika Utekelezaji wa shughuli zao za kawaida
0 Comments