Header Ads Widget

MWENGE WATEMBELEA SHULE YA WENYE MAHITAJI MAALUM MBEYA VIJIJINI.



NA JOSEA SINKALA, MBEYA.

Kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa Godfrey Mzava amewataka wananchi hususani wazazi na walezi kuendelea kushirikiana kulea watoto katika maadili mema watakaokua wakichukia Rushwa ili kuwa na jamii yenye usawa, uwajibikaji na haki kwa maendeleo endelevu.

Pia Mzava amewahimiza wananchi kujitokeza kujiandikisha kwenye daftari la mkazi na baadaye daftari la kudumu la mpiga kura ili kuchagua viongozi bora wakati utakapowadia.

Kiongozi huyo amesema hayo wakati akizungumza na wanafunzi wa shule ya msingi yenye watoto wa mahitaji maalum katika kata ya Nsalala Mbalizi, viongozi na wananchi mbalimbali waliojitokeza kwenye mwendelezo wa mbio za mwenge ambazo zimefanyika katika Halmashauri ya Mbeya.

Amekagua shule hiyo ambayo imejengwa na Halmashauri ya Mbeya na kuanza mwaka jana ambapo pamoja na mengineyo amezindua club ya wapinga Rushwa shuleni hapo.

"Niwapongeze sana watoto wazuri na walimu pia, hii shule imefunguliwa na mwenge mwaka jana na mwaka huu mmeanzisha club ya wapinga Rushwa watoto wakike hamsini na wakiume hamsini kwakweli ni jambo zuri ili kuwafanya watoto wakue wakijua Rushwa ni mbaya na inaharibu haki za watu hivyo tuendeleze utamaduni huu na inawezekana kuwa na idadi kubwa zaidi ya watoto na kuendelea kuwaambia madhara ya kutoa na kupokea Rushwa", amesema Mzava.

Wakimbiza mwenge hao, wanasema kupitia chaguzi zijazo mtu akipita kwa kutoa Rushwa hawezi kuwa na uchungu wa kuwaletea wananchi maendeleo badala yake atajikita kwenye kurejesha fedha alizohonga ili achaguliwe.

Mbunge wa jimbo la Mbeya vijijini Mhe. Oran Njeza ameishukuru Serikali kwa kuendelea kutoa fedha na kuwekeza kwenye elimu ambayo ni sekta muhimu katika kuwa na Taifa lenye wasomi kwa maendeleo yao na Taifa kwa ujumla.

Mbunge Njeza amesema Serikali ya awamu ya sita imetoa mabillion ya fedha kwa ajili ya utekelezwaji miradi mbalimbali katika jimbo lake hilo na kuwaomba wananchi wenzake kuendelea kujiandaa kushiriki uchaguzi wa Serikali za mitaa l, vitongoji na vijiji kwa kuchagua viongozi bora kwa maendeleo yao.

Gloria Gasper ni mwenyekiti wa club ya wapinga Rushwa Rushwa katika shule ya msingi Muungano na mwanafunzi wa shuleni hapo, anasema Rushwa ni wajibu wa kila mtu kuhakikisha inatokomezwa katika jamii ili kujenga jamii yenye maadili.

Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya mkoani Mbeya kupitia afisa elimu msingi mwalimu Tanu Kameka kwa niaba ya mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri hiyo, anasema shule hiyo ina wanafunzi 585 wenye mahitaji maalum lengo kuu likiwa ni kuwapa fursa watoto wenye mahitaji maalum ikiwemo kupata haki yao ya kielimu.

Katika ziara hiyo kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa amegawa kofia na mafuta kwa baadhi ya watoto wenye ulemavu wa ngozi ili kuwasaidia kusoma na kuishi kwenye mazingira rafiki.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI