Na Fredrick Siwale -Matukio Daima APP Mufindi.
HALMASHAURI ya Mji Mafinga mkoani Iringa, imepaa katika ukusanyaji wa mapato ya ndani kutoka Tsh.Bilioni 5,5 mwaka 2023/2024 hadi T.sh .Bilioni 6,2 sawa na asilimia 113.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji Mafinga Bi.Fidelica Myovella katika kikao cha Baraza la madiwani uliofanyika juzi katika Ukumbi wa Halmashauri ya Mji Mafinga.
Mkutano huo ulikusudia kujadili taarifa za kipindi cha mwaka wa fedha 2023 na 2024 na kuhudhuriwa na Viongozi mbali mbali akiwapo Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Dkt .Linda Salekwa,Katibu Mkuu wa CCM Wilaya ya Mufindi Ndugu Clemence Bakuli, Madiwani na Wakuu wa Idara.
Aidha Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Dkt .Linda Salekwa ametoa pongezi kwa Viongozi wa Mji Mafinga pamoja na kuwaasa kuendelea kuwa waadilifu na kuongeza ufanisi na bidii katika kazi .
Pia itaka Halmashauri hiyo kuchapa kazi kwa Vitendo kwani tayari T.sh.Bilioni 2 zimetoewa na Serikali kwa ajili ya mradi wa elimu kwa Shule za msingi na Sekondari katika Wilaya hiyo.
Wakati huo huo Halmashauri ya Mji Mafinga kupitia kitengo cha habari na mawasiliano chini ya Afisa habari Bi.Sima Bingileki imepata cheti na tuzo kwa kushika nafasi ya 6 kati ya Halmashauri 184 zilizo shindanishwa hapa Nchini.
0 Comments