Na Shemsa Mussa -Matukio daima App
Kagera.
KATIBU mkuu wa Chama Cha mapinduzi (CCM) Dkt Emmanuel Nchimbi amewashukuru wananchi wa wilaya ya Kyerwa mkoani Kagera kwa kuendelea kuwa na Imani na Chama hicho huku aliwaomba kuendelea kuwa na Imani na serikali ya awamu ya sita chini ya CCM.
Kuhusu kero ya Miundo mbinu ya barabara ameagiza changamoto hizo Kufanyiwa kazi.
Dkt Nchimbi amewashukuru wananchi wilaya ya Kyerwa na Wana CCM wote kwa Kumpokea na kujitokeza kwa wingi katika Mkutano wake na kusema kuwa katika suala la Vitambulisho vya Taifa ameahidi kumtuma Mhe Waziri wa Mambo ya Ndani kuja wilayani Kyerwa kuona na kutambua nini shida hasa inayokwamisha zoezi Hilo huku akisema Serikali inaendelea kutatua changamoto ndogondogo ili kuhakikisha Kila Mtanzania aweze kupata kitambulisho.
Akizungumza mbele ya Katibu Mkuu Dkt Emmanuel Nchimbi, Mhe Innocent Bilakwate Mbunge wa wilaya ya Kyerwa wakati aliposimama na kuzitaja changamoto zinazowakabili wananchi wilayani humo na kumesema kuwa changamoto ya miundombinu ya Barabara imekuwa kero ya muda mrefu kwao.
Mhe Bilakwate ameongeza kuwa changamoto nyingine ni ukosefu wa vitambulisho vya Taifa (NIDA) kwa wananchi wa wilaya ya Kyerwa , tatizo la ukosefu wa maji pamoja na ukosefu wa umeme wa uhakika Hali inayopelekea wananchi kukosa Maendeleo na kutokuwa kwa wilaya hiyo.
Akijibu baadhi ya kero Waziri wa Ujenzi Mhe Innocent Bashungwa ambaye pia ni Mbunge wa wilaya ya karagwe amesema kuhusu Barabara kutoka Omurushaka hadi Makao Makuu ya wilaya ya Kyerwa tayari mchakato wa Ujenzi umekamilika na Ujenzi utaanza hivi karibuni pia amesema baada ya ujio wa Katibu Mkuu kuisha atarudi kyerwa kwa ajili ya kukamilisha taratibu zote na kuanza Ujenzi
Ikumbukwe kuwa Dkt Nchimbi alianza ziara yake ya kikazi Mkoani Kagera katika wilaya ya Biharamulo na ataongea na wananchi na kuzitembelea wilaya zote zilizomo Mkoani humo,huku akiwa ameambatana na Viongozi mbalimbali wa Serikali pamoja na chama Cha Mapinduzi CCM.
0 Comments