Header Ads Widget

ZOEZI LA UBORESHAJI DAFTARI LA MPIGA KURA KUANZA RASMI KAGERA

 


Na Shemsa Mussa_KAGERA.


Tume huru ya Uchaguzi imewataka wananchi Mkoani Kagera kujitokeza katika zoezi la Uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura ambalo litaanza Agost 5 Mwaka huu.


Hayo yamezungumzwa na Makamu Mwenyekiti wa TumeTaifa ambaye pia ni jaji Mstaafu wa Mahakama ya ( Rufani ),Mhe. Jaji Mbarouk S Mbarouk ambae alikuwa mgeni rasmi katika Mkutano wa Tume na wadau wa uchaguzi kuhusu uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura uliofanyika katika ukumbi wa Mkuu wa Mkoa Kagera. 


 Amesema uzinduzi wa uboreshaji wa daftari la kudumu la mpiga kura lilifanyika julai 20 Mwaka huu Mkoani Kigoma, ambapo mzunguko wa kwanza wa daftari Hilo umeanzia kigoma ,Tabora na katavi hivyo na Mzunguko wa pili unatarajiwa kuanza mwezi Augost 5 katika Mkoa wa Kagera na Geita.


Nae Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Uchaguzi Giveness Aswile ambaye ni Mkurugenzi wa idara ya habari na elimu ya mpiga kura amesema kupitia uboreshaji wa daftari hilo katika,Mkoa Kagera unatarajiwa kuandikisha wapiga kura wapya 2,29,321 ikiwa ni ongezeko la asilimia 15.5 ya wapiga kura 1,412,008 waliopo kwenye daftari la kudumu la wapiga kura.


Hivyo tume inatarajia baada ya uandishaji katika Mkoa wa Kagera utakuwa na jumla ya wapiga kura 1,631,329 pia amezitaja sifa za mpiga kura na ambaye hana sifa ya kuboresha taarifa zake katika daftari la kudumu la mpiga kura.


" Sifa ya kwanza katika zoezi hili lazima mpiga kura awe raia wa Tanzania na awe na umri kuanzia miaka 18 na kuendelea na Kuna Watanzania unakuta Wana miaka mingi mfano kama 75 lakini Hajawai kujiandikisha watu wa namna hiyo hawazuiliwi na sisi hatumzuii kuja kujiandikisha maana zoezi hili na jambo hili ni hiyari ya mtu na Uzalendo, amesema Bi Giveness"


Sambamba na hayo ameyasihi makundi mbali mbali wakiwemo wanawake, vijana wazee wa kimila ,Viongizi wa dini pamoja na vyombo vya habari, kuweka Uzalendo mbele na kutumia muda huo kuwakumbusha na kuwahamasisha wananchi juu ya Umuhimu wa kujihandikisha katika daftari la mpiga Kura.


Nao baadhi ya washiriki katika kikao hicho akiwemo Bw Hermes Peter Nyarubamba ambaye ni Mwenyekiti wa Machifu na Viongizi wa kimila Mkoani humo ameeleza kufurahishwa na zoezi Hilo kutokumbagua mtu wa aina yoyote huku akisema kuwa ni jambo jema kuwashirikisha watu waliopo magerezani (Wafungwa) pamoja na makindi maalimu wakiwemo watu wenye ulemavu.


Pia Bw Nyarubamba ameongeza kwa kuwasisitiza Machifu wenzake kutoa elimu Bora kwa wananchi ili kujua umuhimu wa kujiandikisha na umuhimu wa kutoa taarifu katika daftari la mpiga Kura.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI