Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE
Jeshi la Polisi mkoani Njombe linawashikilia watu 4 kwa mahojiano juu ya mauaji ya Bibi Tulivane Mkongwa [85] mkazi wa Idundilanga aliyefariki kwa kukatwa kichwani na kitu chenye ncha kali huku mtuhumiwa wa tukio hilo Petro Mhenga mfanyakazi wake wa Ng'ombe akiendelea kutafutwa.
Tukio hilo limetokea julai 20 mwaka huu mjini Njombe huku Imani za Kishirikina ni sababu iliyotajwa na Kamanda wa Polisi mkoa wa Njombe Mahamoud Banga kuwa bibi huyo amekuwa akihusishwa na ushirikina katika mtaa wa Idundilanga Chauginge huku akiwataja wanaoshikiliwa kuwa ni pamoja na Watoto wa Marehemu Anna Mmelo [61] mkazi wa Nazareth,Devotha Mmelo[49] ambaye ni mwalimu na sababu ya kuwashikilia ni kutokana na kushiriki kufanya usafi wa nyumba,Nguo na mwili wa marehemu kabla ya polisi kufika eneo la tukio.
Wengine wanaoshikiliwa na Polisi ni Magreth Idoa [32] mkazi wa Idundilanga na Marko Msigwa[40] mkata majani ya Ng'ombe huku anayetafutwa ni kutokana na kutokuwepo nyumbani hapo siku ya Tukio.
Mamia ya wananchi waliofika katika eneo la tukio wamegubikwa na simanzi kutokana na namna walivyoishi na Bibi huyo huku Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Idundilanga Filoteus Ngilangwa akisema alipigiwa simu na msamaria mwema kumfahamisha juu ya tukio hilo na ndipo alipofika nyumbani hapo.
Kufuatia sintofahamu hiyo baadhi ya wananchi wanaoishi mtaa mmoja na marehemu akiwemo Florah Msemwa na Magreth Mwenda wameeleza namna walivyokuwa wanamfahamu na walivyoishi naye.
Mwili wa marehemu ulipelekwa Katika chumba cha kuhifidhia maiti Kibena Hospitali kwa ajili ya uchunguzi zaidi wa Daktari na Maziko yatafanyika baada ya taratibu zote kukamilika.
0 Comments