Header Ads Widget

WAKULIMA WA KAHAWA YA KILIMO HAI MSAE KINYAMVUO KULIPWA

 


NA WILLIUM PAUL, MOSHI. 


WAKULIMA wa kahawa ya Kilimo Hai ambao ni wanachama wa Chama cha Msingi cha Ushirika cha Msae Kinyamvuo ambao mnamo Julai 27 mwaka 2022 waliingia mkataba na makubaliano na KNCU ya kuuza kahawa hiyo kwa kampuni ya Continental Trade and Commodity Service (CTCS) kwa  shilingi 11,250 bila mafanikio. 


Serikali iliunda kamati maalum ambayo iliundwa na waziri wa Kilimo Hussein Bashe kuchunguza madai hayo ambayo ilitoa ripoti yake iliyoonesha kweli wakulima hao walidhulumiwa na hatua za kinidhamu zichukuliwe kwa watendaji wa KNCU ikiwemo kuwasimamisha kupisha uchunguzi pamoja na TAKUKURU kuchunguza jambo hili ili kuwafikisha mahakamani. 



Akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara eneo la Mrimbo Uuo kata ya Mwika Kaskazini Naibu Waziri wa Kilimo David Silinde amewahakikishia wakulima hao ya kwamba tayari Wizara yao ya Kilimo kwa kushirikiana na Bodi ya Kahawa pamoja na Tume ya Ushirika wamekubaliana kulipa fedha hizo kiasi cha takribani shilingi milioni 461 ndani ya muda mfupi toka sasa. 


Uamuzi huo uliibua shangwe kubwa  na pongezi toka kwa wananchi. 



Naye Mbunge wa Jimbo la Vunjo Dkt Charles Stephen Kimei amesema anamshukuru kwa dhati Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa serikali anayoiongoza kuridhia kuwalipa wakulima hao wa kahawa kwani ni kielelezo cha wazi inathamani wananchi na yenye kutenda haki.



Diwani wa Mwika Kaskazini Samwel Shao alimshukuru Mbunge Kimei kwa kuwa mstari wa mbele kupigania jasho la wakulima hao pamoja na Naibu Waziri wa Kilimo Silinde kwa majibu mazuri ya serikali. 



Kwa upande wa Katibu wa CCM Wilaya ya Moshi Vijijini NRamadhan Samwel Mahanyu aliwataka wananchi wa Mwika Kaskazini kuachana na siasa za ulaghai badala yake waendelee kukiamini na kukipa ridhaa Chama Cha Mapinduzi kwa Umoja, Amani na Maendeleo.



Mwisho..

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI