Header Ads Widget

WAKINAMAMA SAME WATAKIWA KUMFUNGA KITENGE RAIS DKT SAMIA SULUHU HASSAN.

 


NA WILLIUM PAUL, SAME.



MBUNGE wa viti maalum kupitia mkoa wa Kilimanjaro, Zuena Bushiri amewataka wakinamama wilayani Same mkoani humo kumfunga kitenge Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kumpa kura za kishindo katika uchaguzi mkuu mwakani. 



Zuena ametoa kauli hiyo wakati akikabidhi mashuka yaliyotolewa na Rais kwa ajili ya kituo cha Afya cha Kisiwani ambapo alisema kuwa, Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya mambo makubwa katika Taifa hili ikiwemo miradi mikubwa na ya kimkakati kwa Taifa. 



Alisema kuwa, katika kuonyesha wananchi wa wilaya ya same wameridhishwa na kazi za serikali ya awamu ya sita ni kutoa kura za kishindo kwa chama cha Mapinduzi katika uchaguzi wa serikali za mitaa pamoja na uchaguzi mkuu mwakani. 



Aidha Mbunge huyo amewataka wakinamama kujitokeza kuwania nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi wa serikali za mitaa. 



Mwisho..

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI