Header Ads Widget

VIJANA WANUFAIKA TANZANIA YA KITIGITALI WATAKIWA KUSOMA KWA BIDII UGAIBUNI


Na Hamida Ramadhan Matukio Daima app Dodoma


KATIBU  Mkuu Wizara ya Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mohammed Khamis Abdulla amewataka vijana walionufaika na ufadhili wa mafunzo ya muda mrefu awamu ya pili kupitia mradi wa Tanzania ya kidigitali  kwenda kusoma kwa bidi na kupeperusha bendera ya Tanzania kwa uzalendo. 



Pia amewata vijana hao kutambua kuwa chanzo pekee cha mafanikio ni ujuzi na uzoefu hivyo wakalinde maslahi ya Taifa la Tanzania


Katibu mkuu huyo ameyasema hayo leo Julai 12,2024 Jijini Dodoma kwenye hafla ya kutoa vyeti kwa wanafunzi  Hao wa awamu ya pili huku akiwasisitiza  kuwajibika, kusoma kwa bidii ili wapate vyeti .


" Kila mmoja lazima awe na malengo ambayo yatamuwezesha kutimiza yale wanayopaswa kutekeleza.

 amewasihi kutumia fursa hiyo kutekeleza malengo ya Serikali hivyo lazima watambuwe kuwa Serikali imewalipia kwenda kusoma na sio mkopo, " Amesema .


Na kuongeza "Kwasasa Wizara inajenga vituo vya ubunifu kwenye maeneo ya Zanzibar, Dodoma, Arusha, Tanga, Kilimanjaro, Morogoro, Mbeya, Iringa, Mtwara, Mwanza na Dar es salaam hivyo wanatarajia wakirudi waje kuwezesha vituo hivyo ambavyo vitatumika kuwawezesha vijana kuendeleza bunifu na tafiti zao katika TEHAMA ikiwemo matumizi ya teknolojia zinazoibukia, " Amesema.


Kwa upande wake Mkurugenzi wa chanzo cha Diaspora kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Salvatory Mbilinyi akitoa mwogozo juu ya mambo wanayopaswa kufanya wawapo nje ya nchi amewaisitiza wanufaika wa mradi huo kutii na kufuata sheria za nchi pamoja na vyuo ambavyo wanaenda ili waweze kutimiza malengo yao kwa manufaa ya taifa, familia pamoja wao binafsi.


Sambamba na hilo amewahimiza kuwa wavumilivu na changamoto zote kipindi wapo masomoni pamoja na kulinda tamaduni za kitanzania kwa kuzingatia maadili na siyo kujisahau wanapokutana na tamaduni za nje ya nchi.



" Nendeni mkasome kwa bidii maana ukweli ni kwamba ukiwa mtoto wa mama nje ya nchi masomo yatakushinda utarudi hivyo mkakaze buti na msipoteze nafasi hii mliobahatika kuipata, " Amesema 

Mwisho





 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI