Header Ads Widget

TANROADS MBEYA KUANZA UJENZI WA BARABARA YA MBALIZI IWALA IHOMBE.

 





Mbunge wa Mbeya vijijini.

Kaimu meneja wa TANROADS mkoa wa Mbeya

NA JOSEA SINKALA, MBEYA.

Wakala wa ujenzi wa barabara Tanzania TANROADS mkoa wa Mbeya umesema unatarajia kuanza ujenzi wa barabara ya Mbalizi Iwala Ihombe kuanzia katikati mwa mwezi ujao (Agosti 2024) ili kusaidia kuboresha huduma za usafiri na usafirishaji wa mazao na abiria hasa wajawazito kufuata huduma za afya mjini Mbalizi.


Hayo yameelezwa na Kaimu meneja wa TANROADS mkoa wa Mbeya Mhandisi Fransisco Mbaza, wakati akizungumza na wananchi wa kitongoji cha Ihombe kata ya Utengule Usongwe mamlaka ya mji mdogo wa Mbalizi kwenye mkutano wa Mbunge wa Mbeya vijijini na wananchi wake hao.


Mhandisi Mbaza baada ya kusikia hoja za wananchi namna wanavyosumbuka kusafiri kwenda Mbalizi kufuata huduma za kiafya na kusafiri mazao yao, amesema Serikali imeweka kwenye mpango barabara hiyo ili ipitite kwa urahisi zaidi.


Amesema kwa kuthamini umuhimu wa barabara hiyo kutoka Mbalizi hadi vitongoji vya Ihombe na Iwala imepasishwa hadi na kujengwa na TANROADS (wanaojenga barabara za mkoa na kitaifa) badala ya Wakala wa barabara mjini na vijijini TARURA (wanaojenga barabara za kiwilaya).


Amesema tayari TANROADS mkoa wa Mbeya imetafuta mkandarasi ambaye mwezi ujao katikati anatarajiwa kuanza utekelezaji wa barabara ya Mbalizi Iwala Ihombe kwa kiwango cha changarawe ili ipitike kwa urahisi.


Mbunge wa Mbeya vijijini Mhe. Oran Manasse Njeza, amesema barabara hiyo ni muhimu kwa wananchi hao ikilinganishwa na kwamba wananchi wake hao ni wakulima wa mazao mbalimbali ikiwemo mahindi na kahawa.


Mbunge Njeza amewataka wahandisi hao wa barabara kutilia manani na kumsimamia mkandarasi ili kutekeleza mradi huo kwa wakati na kiwango ili kuwasaidia wananchi wake hasa wa maeneo ya vitongoji vya Ihombe, Iwala na mji mdogo wa Mbalizi pia ili pia kukuza uchumi wao na Serikali kwa ujumla.


Wananchi wa vitongoji vya Ihombe na Iwala wanasema wamekuwa wakipata kadhia mbalimbali wanaposafirisha wagonjwa na wajawazito kwenda kituo cha afya Utengule na hospitali teule ya Ifisi Mbalizi.


Nao wakulima wanadai huwa wanalazimika kusukuma mazao yao kwa baskeli kutokana na ubovu wa barabara kutoka Mbalizi hadi Ihombe hivyo kuathirika kiuchumi licha ya kuwa ndio wachangiaji wa mapato ya Halmashauri hivyo ni muhimu miundombinu hiyo ikaboreshwa.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI