Header Ads Widget

RAIS SAMIA AMEONYESHA DUNIA WANAWAKE WANAWEZA KWENYE UONGOZI

 


Na Ashton

 Balaigwa,MOROGORO

MBUNGE wa Jimbo la Morogoro Mjini,AbdulAziz Abood,Amesema

Rais Dk Samia Suluhu Hassan ameionyesha Dunia kwa vitendo  kuwa wanawake wakipewa nafasi  kwenye  uongozi wanawaweza kuleta maendeleo kwenye nchi sawa na wanaume.


Kutokana na umuhimu huo ,Rais Samia Suluhu Hassan ameteua Makatibu Tawala 26 ambapo wanawake 12 sawa na asilimia 46,Majaji 28 kati yao 12 pamoja na baadhi ya wakuu wa mikoa na wilaya wanawake ili kuwapa nafas katika uongozi.


Mbunge Abood alisema hayo wakati akifungua Kongamano la mafunzo kwa wanawake Mkoani Morogoro,lililoandaliwa na Shirika la Wanawake katika Elimu (SWE) lilipo mjini hapa.


Abood alisema kutokana na umahili na uchapakazi wa Rais Samia Suluhu Hassan hivi sasa nchi nyingi Duniani zimeanza kuiga Tanzania kwa kuwapa nafasi za uongozi  wanawake katika maeneo Nyanja mbalimbali hatua ambayo inaanza kuleta mageuzi na kuwafanya wanawake waendelee kujiamini..


“Leo tunaona umuhimu wa kumsomesha au kumwezesha mwanamke,tunashuudia Rais Samia Suluhu Hassan akifanya mambo makubwa katika nafasi ya kuongoza Tanzania kama Rais,mama yetu anapambana sana na maendeleo tunayaona wote hivyo wanawake tembeeni kifua mbele mnaweza sana” alisema Abood.


Alisema Tanzania imeridhia kutekeleza mkataba wa kimataifa wa kutokomeza aina zote za ubaguzi dhidi ya wanawake ili kuhakikisha uwiano sawa kwenye vyombo vya kimaamuzi unapatikana ili kuleta maendeleo.


Hata hivyo Mbunge huyo alisema ili kufikia malengo hayo ya kuwepo kwa uwiano sawa kwa wanawake kwenye uongozi bado elimu juu ya ukatili na unyanyasaji wa kijinsia iendelee kutolewa ili kupinga manyanyaso na aina yoyote ya kuonekana kupinga haki.


Akizungumzia kuhusu kongamano hilo,Abood alihaidi baada ya mafunzo hayo atakaa na kundi hilo la wanawake kwa kushirikiana na taasisi mbalimbali za kifedha ili waweze  kufanya miradi mbalimbali ya ujasilimali ili waweze kujikwamua kiuchumi.


Naye Mtendaji Mkuu wa Shirika hilo la SWE  George Lukoa,alisema wameamua kuwajengea uwezo wanawake hao kwenye masuala ya kisiasa,elimu katika jinsia,ushirikishwaji wa masuala ya mazingira na nishati, safi, ukatili,vita ya kupambana na madawa ya kulevya,elimu ya fedha na ushirikishwaji wa masuala ya kiuchumi.


Alisema maamuzi ya kutoa elimu hiyo inatokana na kuwepo kwa changamoto kubwa kwenye uelewa kwa baadhi ya wanawake hasa kwenye mambo mtambuka hivyo wameamua kuwapa elimu.


Hata hivyo alisema wamegundua wapo wanawake wengi bado hawajajua kuhusu masuala ya kukopa fedha kwenye taasisi hizo na baadhi yao kujikuta wakiingia kwenye mikopo umiza yenye riba kubwa maarufu kama kausha damu na kujikuta wakishindwa kufanya shughuli za maendeleo.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI