Header Ads Widget

NJEZA ASHUSHA NEEMA UBORESHAJI MADARASA SM/IWOWO, KUTOA MOTISHA UFAULU WA A.

 


NA JOSEA SINKALA, MBEYA.


Mbunge wa Mbeya vijijini Mhe. Oran Njeza ameahidi kuchangia fedha kiasi cha shilingi million mbili kwa ajili ya uboreshaji vyumba vya madarasa katika shule ya msingi Iwowo kata ya Itawa Umalila Mbeya vijijini ikiwemo kuweka sakafu kwenye madarasa shuleni hapo.


Njeza ametoa kauli hiyo baada ya kutembelea shule hiyo wakati akiendelea na ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo na kuzungumza na wananchi na wanafunzi mashuleni.



Akiwa shuleni hapo Njeza amewasisitiza wanafunzi kusoma kwa bidii ili kufikia ndoto zao.


Katika kuwaunga mkono ameahidi kuendelea kununua ufaulu wa alama A kwa wanafunzi wote wa darasa la saba watakaofanya vizuri akiahidi kutoa shilingi laki moja kwa wanafunzi wote wa darasa la saba watakaopata A kwa masomo yote.



Pia amechangia shilingi laki tatu kwa ajili ya kuhakikisha wanafunzi hao wanaendelea kupata chakula cha mchana shuleni ili kuinua ufaulu kwa watoto hao.


Pamoja na hayo ameahidi kutoa shilingi million mbili kwa ajili ya kuboresha sakafu shuleni hapo kutokana na baadhi ya madarasa kutokuwa na hali nzuri ambapo katika kuongeza ufaulu ameahidi shilingi laki sita kwa ajili ya shule za msingi Iwowo na Igalukwa kata ya Itawa.


Mbunge wa Mbeya vijijini Mhe. Oran Manasse Njeza, anaendelea na ziara katika kata mbalimbali za jimbo lake ili kuendelea kukutana na wananchi wake katika utekelezaji wa ahadi zake kwenye ilani ya CCM ya mwaka 2020-2025 ikiwemo kwenye idara ya elimu.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI