Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE
Chama cha mapinduzi CCM mkoa wa Njombe kimeelekeza kuwekwa watu wazuri na wanaokubalika katika jamii ili waweze kugombea nafasi mbambali za uongozi kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa baadaye mwaka huu na uchaguzi mkuu hapo mwakani.
Agizo hilo limetolewa na Katibu wa Itikadi siasa Uenezi na mafunzo CCM mkoa wa Njombe Josaya Luoga katika mkutano mkuu wa Ccm tawi la Mjimwema ambapo amesema Wakati wakipanga mikakati mbalimbali ya ushindi ni lazima kuwaweka watu wanaokubalika zaidi katika jamii.
Awali taarifa ya Utendaji kazi ya CCM tawi la mjimwema iliyosomwa na katibu tawi Emmanuel Mkane imeeleza mafanikio makubwa ya ujenzi wa miradi ikiwemo ofisi na kilimo cha miti itakayosaidia pato kupanda katika tawi lao.
Serikali ya mtaa wa Mjimwema chini ya mwenyekiti wake Lenard Mkupi na Mtendaji wake Izack Mwakyusa imeeleza kuwa miradi mbalimbali ya maendeleo zikiwemo shule,Zahanati na Ofisi imeendelea kutekelezwa kutokana na serikali kupeleka fedha.
Wakati miundombinu ya elimu ikiendelea kujengwa Katika kata hiyo Mgeni wa heshima katika mkutano huo Angela Mwangeni Diwani wa viti maalumu tarafa ya Njombe mjini Amewataka wazazi kuwalinda watoto wao dhidi ya ukatili kwani hali ni mbaya nchini Tanzania.
Baadhi ya wananchi wa mtaa wa Mjimwema akiwemo Irene Makinda na Atu Msambwa wanakiri kuwapo kwa taarifa za vitendo vya ukatili kwa watoto na kwamba ni jukumu la kila mzazi katika mapambano dhidi ya ulawiti,Vipigo,Ubakaji na utelekezaji watoto.
Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Sinai Mjimwema licha ya kukana kuwapo kwa vitendo vya ukatili kwa wanafunzi shuleni lakini anawataka wazazi kuwa makini katika malezi ya watoto wao.
Vitendo vya ukatili wa kijinsia vinapaswa kupingwa na kila Mtanzania ili kuwalinda watoto.
0 Comments