Header Ads Widget

MPETE DIWANI CUP YAHAMASISHA VIJANA KUSHIRIKI UCHAGUZI NJOMBE

Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE


Vijana mkoani Njombe wamehamasishwa kujitokeza kushiriki vyema katika uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika  mwaka huu na uchaguzi mkuu hapo mwakani.


Katika uzinduzi wa Ligi ya  Mpete Diwani Cup Diwani wa kata ya Utalingolo Halmashauri ya mji wa Njombe Mhe.Erasto Mpete ambaye ni mwenyekiti wa halmashauri amesema ni fursa kwa vijana kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali katika uchaguzi wa serikali za mitaa.


Aidha Mpete amesema mashindano hayo yanayofanyika katika viwanja vya Ruhuji Utalingolo yamekuwa yakifanyika kila mwaka na yamelenga kuwakutanisha vijana na kuwaunganisha katika fursa mbalimbali pamoja na kuwahamisha kugombea katika nafasi mbalimbali.


Mgeni wa heshima katika uzinduzi wa Ligi hiyo Erasto Ngole ambaye ni mkurugenzi wa kampuni ya Shkamoo Parachichi amesema taifa linahitaji nguvu kazi hivyo vijana kupitia uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu ujao wanayo nafasi kwa kugombea.

Baadhi ya wachezaji akiwemo Baraka Fulgecy toka Utalingolo Fc na Evaristo Mkalawa toka Ihalula Fc wanakiri kuwa michezo ni fursa kubwa kwao na inawaunganisha wakiwa vijana kuelekea katika uchaguzi wa serikali za Mtaa.


Aidha vijana hao wamesema ligi hiyo itawasaidia  kujiepusha na makundi hatarishi kwa kuwa watakuwa wanajishugulisha na michezo nyakati ambazo watakuwa hawana kazi.


Timu nne Kwa muda wa wiki mbili Utalingolo Fc Ihalula Fc Nole Fc na Mfereke Fc ndizo zilizoanza kutimua vumbi katika ligi hiyo itakayokwenda kwa muda wa wiki mbili



 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI