MBUNGE wa viti maalum kupitia mkoa wa Kilimanjaro, Zuena Bushiri amekabidhi bendera za Chama cha Mapinduzi kwa kamati ya Siasa wilaya ya Moshi mjini ili kuzipeleka kwa mabalozi kuhamasisha wananchi kushiriki katika uchaguzi wa serikali za mitaa.
Zuena alisema kuwa, lengo la kutoa bendera hizo kwa mabalozi ni kuwatia motisha wa kwenda kuwashawishi wananchi kujitokeza kwa wingi kushiriki chaguzi za serikali za mitaa.
"Mabalozi ni watu mahimu kwa Chama chetu kwani wao ndio wenye wananchi ambapo muda wote wanakuwa nao hivyo tunawaomba sana wahamasishe wananchi kushiriki kwa wingi kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa badae mwaka huu" Alisema Zuena.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi wilaya ya Moshi mjini, Faraji Swai alimshukuru Mbunge huyo kwa kuonyesha kuwajali mabalozi pamoja na Chama na kuahidi kupata ushindi wa kishindo katika uchaguzi huo.
Mwisho.
0 Comments