Header Ads Widget

HALMASHAURI WILAYA YA IKUNGI YAHITAJI BIL.11/- KUKARABATI MIUNDOMBINU

  

Na Thobias Mwanakatwe,IKUNGI

HALMASHAURI ya Wilaya ya Ikungi mkoani Singida inahitaji zaidi ya Sh.Bilioni 11 kwa ajili ya ukarabati wa miundombinu ya sekta ya elimu,afya na ofisi za serikali za vijiji na kata.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi,Justice  Kijazi, alisema hayo juzi kwa nyakati tofauti katika ziara yake ya kusikiliza kero za wananchi na watumishi kwenye kata za Misughaa, Kikio na Ntuntu.

Alisema katika halmashauri hiyo kuna baadhi ya shule hakavu zinazohitaji kukarabatiwa, ujenzi wa madarasa, m ofisi za serikali za kata na vijiji na zahanati ambapo ili kukamilisha ujenzi huo kunahitajika kiasi hicho cha fedha.

Kijazi alisema katika kuhakikisha fedha hizo zinapatikana, katika mwaka wa fedha wa mwaka huu halmashauri imeanga kutenga kidogo kidogo katika mapato yake ya ndani wakati nyingine zipatikana kutoka serikari kuu,wafadhiri na wadau mbalimbali wa maendeleo.


Alisema katika Kata ya Misughaa halmashauri imetenga Sh.milioni  80 kwa ajili ya kutatua kero mbalimbali ambapo kati ya hizo  Sh.milioni 20 zitatumika kumalizia ujenzi wa bweni la wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Dk.Sheni.



Katika shule hiyo, Waziri wa Habari na Teknolojia ya Habari, Nape  Nnauye, alitoa mchango wa saruji mifuko 400 kukamilisha ujenzi wa bweni la shule hiyo.


Aidha,Kijazi  aliagiza ujenzi wa vyoo vya  zahanati ya Misughaa ukamilike haraka ili kupunguza adha iliyopo na kukarabati baadhi ya vyumba vya madarasa pamoja na kuhakikisha madawati yanatosheleza kwa wanafunzi.



Alipongeza juhudi za shule ya Sekondari Dkt sheini kutekeleza maagizo ya serikali ya wanafunzi kupata chakula wakiwa shuleni kwani wananchi wametekeleza kwa kiwango kikubwa na wana akiba ya chakula cha kutosheleza mpaka mwaka 2025.


Naye Afisa Utumishi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi, Jonas Lutiga amesisitiza watumishi kufuata maadili ya kiutumishi kuanzia nidhamu ya mavazi na utekelezaji wa majukumu yao ya serikali ili kukuza maendeleo katika halmashauri hiyo.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI