Header Ads Widget

DC MOYO AAGIZA KUKAMATWA WANAFUNZI WATORO NA KURUDISHWA SHULE.

Mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo ameagiza kusakwa kwa wanafunzi wote watoro katika shule zote na kuchukuliwa hatua za utoro 

Akizungumza kwenye moja ya ziara zake alisema kuwa haiwezekani wanafunzi wanaanza kusoma wengi halafu ghafla wengi wanaacha shule bila kuwa na sababu za jambo ambalo ni hatari kwa taifa hapo baadaye.


Moyo alisema kuwa haiwezekani wanafunzi awe mtoro halafu wazazi,walezi wasijue hivyo ametoa amri familia yoyote ile itakayowakumbatia wanafunzi watoro watachukuliwa hatua kali za kisheria.


Moyo alimazia kwa kusema kuwa haiwezeka Tanzania ikiwa na wananchi ambao sio wasomi wakati serikali inatoa elimu bure kuanzia darasa la kwanza hadi kidato cha nne hiyo ni aibu kwa wilaya na hatakubali kutokea kwa jambo hilo.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI