Mwenyekiti wa ngome ya vijana (Taifa) wa chama cha ACT Wazalendo Abdul Nondo, Juni 26, 2024 akikiwakilisha chama chake cha ACTwazalendo na Ngome yaVijana, ameshiriki mazishi ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Ngome ya vijana mkoa wa Tanga Charles James Mdoe akiwa ameambatana na viongozi wa Mkoa wa Tanga, jimbo na wanachama wengine mbalimbali kwenye msiba huo na kutoa salamu za rambirambi.
Pamoja na hayo Nondo ametoa salamu za Chama hicho pamoja na Ngome ya vijana kwa familia ya marehemu aliyekuwa kiongozi wa vijana wa chama hicho cha upinzani katika mkoa wa Tanga ambapo maziko yamefanyika jumatano hii katika wilaya ya Korogwe mkoani Tanga.
0 Comments