Na Hamida Ramadhan Matukio Daima Blog
MAWAKILI wote wa Serikali hapa nchini wametakiwa kutenga muda na kuwasiliza wananchi katika maeneo yao kupitia kamati za ushauri wa kisheria ngazi za Mikoa na Wilaya zilizozinduliwa na Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji Dkt, Eliezer Feleshi ameyasema hayo leo Juni 36 ,2024 Jijini Dodoma katika siku ya Uzinduzi wa Kliniki ya Ushauri na Elimu ya Kisheria kwa Umma.
Amesema maelekezo hayo ya Waziri Mkuu yalitolewa katika mkutano wa Chama cha mawakaili wa Serikali uliofanyika Machi, 21 2024 Katika ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete Dodoma.
Jaji Feleshi amesema Kliniki hiyo ni matokeo ya wajibu wa kikatiba inaoitaka Serikali kuwajibika katika masuala ya wananchi wake.
" Kwakuwa Serikali inawekwa madarakani na watu hivyo Serikali kupitia ofisi yangu inayo wajibu wa kushugulikia masuala ya wananchi, " Amesema Jaji Feleshi.
Aidha Jaji Feleshi ametumia fursa hiyo kuwakumbusha wakuu wa Mikoa na Wilaya zote nchini ambazo bado hawajakamilisha kuteua wajumbe wawili wa kamati za ushauri ngazi za Mikoa na Wilaya kwa Mujibu wa mwongozowa wa huduma za ushauri wa kisheria ngazi za Mikoa na Wilaya kufanya hivyo ili kamati hizo zianze kazi ya kusikiliza Malala Mikoa wananchi kwa kuzingatia utaratibu utakaowekwa.
" Navikumbusha Vyama vya Mawakaili Serikalini (TPBA) pamoja na Chama cha Mawakaili wa Tanganyika (TLS) kuendelea kushirikiana na Serikali, kamati za ushauri wa kisheria ngazi za Mikoa na Wilaya ili kusikiliza Malalamiko ya wananchi, " Amesema Jaji Feleshi
Hata hivyo amesema Kliniki zitakazoendeshwa na kamati hizo zitakuwa endelevu kwa nchi nzima ambapo Mawakaili wa Serikali na wadau katika utoaji wa Masada wa kisheria watatoa huduma katika maeneo yao.
Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Mary Makondo ameeleza kuwa wananchi wakiendelea kutatuliwa kero zao uzalishaji utakua kwa kasi.
Amesema Serikali kupitia kampeni ya msaada wa kisheria ya Mama Samia wananchi wamekuwa sehemu ya mabadiliko kwa kuelewa namna ya kutafuta suluhu ya malalamiko yao.
"Kero za wananchi ni wajibu wetu, tuendelee kuwa pamoja katika kuzitatua kupitia ushirikiano wetu, kupitia hizi siku zilizotengwa wananchi wataendelea kuzitumia vizuri kuelimishwa zaidi ili wapate haki yao na kuwa na amani, " amesema
Amesema wataendelea kuboresha mifumo ya msaada wa kisheria kupitia digitali na simu za kawaida ili kufanikisha huduma bora kwa wananchi.
Mwisho
0 Comments