Header Ads Widget

BREAKING:WAFANYABIASHARA IRINGA WAFUNGUA MADUKA













 Baadhi ya wafanyabiashara wa maduka mjini Iringa ambao Jana hawakufungua maduka leo wamefungua maduka yao huku wakidai mgomo Wao umekosa nguvu baada ya kukosa msukumo wa viongozi wa Jumuiya ya wafanyabiashara Tanzania(JWT) mkoa wa Iringa.

Matukio Daima media imeshuhudia maeneo mbali mbali yakiwemo ya Miyomboni ambayo ni maeneo maarufu mjini Iringa kwa biashara  maduka mengi yakiwa yamefunguliwa .


Zoezi la kufungua Maduka lilionekana kuongezeka zaidi kati ya saa 2:30 Hadi saa 3 asubuhi ambao ni muda wa wafanyabiashara wengi kufika mjini hapa .

Awali mida ya saa 1 asubuhi ni maduka machache zaidi yalikuwa yamefunguliwa huku Kila mmoja akisubiri kuona wengine kama wanafungua ila idadi hiyo imeendelea kuongezeka hadi majira ya saa 3:20 mwandishi wa habari wa Matukio Daima media akiondoka eneo hilo .


Sarah Sanga ni mmoja kati ya wafanyabiashara wa maduka eneo la Miyomboni amesema kuwa mgomo wao hauna nguvu hivyo ameona ni vema kufungua Duka kuendelea na kazi .


Wakati John Kalinga akidai kuwa JWT wamekuwa nyuma zaidi kuhamasisha mgomo huo hivyo kuendelea Kufunga maduka ni kupisha na gari la mshahara.


"Hatufungi tena maduka bila Kuwepo taarifa sahihi ya kwanini tufunge maduka hii ya Jana haikueleweka vizuri wengine tulifunga wangine wamepiga kazi kama kawaida"


Mapema Jana akizungumza na Matukio Daima Tv kwenye kipindi Cha Tanzania ya leo katibu wa Jumuiya ya wafanyabiashara Tanzania (JWT)mkoa wa Iringa Cola Benitho alisema hakuna mgomo wa wafanyabiashara Iringa hivyo Waliofunga maduka ni uamuzi Wao na wale Waliofunga hakuna adhabu yoyote maana JWT hawajatoa tamko la mgomo.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI