NAIBU Waziri Mkuu Dkt. Dotto Biteko ameonyesha kufurahia kuanzishwa kwa huduma ya Bima ya mifugo iliyotambulishwa na Banki ya NMB wakati akiwa katika banda la maonyesho la banki hiyo akikagua mabanda maonyesho ya tatu ya Jumuiya ya Wafugaji kibiashara nchini TCCS katika viwanja vya Ubena Estate huko Ubena Zomozi Halmshauri ya Chalinze mkoani Pwani alipofika kufunga maonyesho hayo.
Alisema huduma ya Bima kwa mifugo ni kitu kikubwa kwa wafugaji na kuwa pongeza Banki ya NMB kwa kutambulisha huduma hiyo na kuwataka wa watoe elimu zaidi kwa wafugaji.
Dkt Biteko alihoji maswali kadhaa Mkuu wa Idara ya Kilimo wa Banki ya NMB Christopher Mwalugenge aliyekuwa akitoa utambulisho huo wa huduma ya Bima kwa mifugo waliyoitambulisha akitakakujua idadi ya wafugaji ambao tayari wameanza kunufaika na huduma hiyo muhimu ambayo itawasaidia Wafugaji iwapo watapatwa na majanga mbalimbali katika ufugaji wao.
Ndipo Mwenyekiti wa Jumuhiya ya wafugaji Kibiashara Nchini TCCS Naweed Mula alisema yeye tayari amekatia bima hiyo kwa mifugo 150 ambayo inamuhakikishia usalama wa mifugo yake ikipatwa na majanga mbalimbali.
Akitambulisha huduma hiyo ya Bima kwa Mifugo alisema Bima hiyo itamsaidia Mfugaji kibiashara kulipwa fidia iwapo mifugo yake itapatwa na majanga mbalimbali katika ufugaji wao ikiwa ni pamoja na kuwezeshwa kuweka miundo mbinu ya kufuga kibiashara kwa idadi ya ng’ombe atakaokuwa nao ili maweze kufuga kibiashara pamoja na kujengewe majosho na miundombinu mingine ya ufugaji.
Mwalugenge alisema huduma hiyo ya bima kwa mifugo huanzia bei ya shilingi 20,000 kwa mfugo ambayo inatoa kinga dhidi ya vifo vya mifugo vitanyotokana na radi, majeraha ya ndani na nje kwenye eneo la usafiri, moto, dhoruba, kung'atwa na nyoka, mafuriko, magonjwa ya asili na yasiyodhibitika kwa mifugo.
Aidha akizungumzia huduma ya mikopo iliyotolewa na NMB katika kipindi cha miaka mitatu NMB Mwalugenge alisema imetoa mikopo ya zaidi ya shillingi Bililoni 316 katika kuwawezesha Wafugaji wafuge kibiashara ambapo pia wanatoa mafunzo ili kupata uhakika wa masoko ya kimataifa katika mnyololo wa thamani.
0 Comments