Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE
Wakati Tanzania ikiungana na mataifa mengine kusherekea siku ya wauguzi duniani,Mganga mkuu wa halmashauri ya mji wa Njombe Dokta Jabir Juma amewaonya wauguzi wenye tabia mbaya ya kuwatukana wagonjwa.
Kwa niaba ya mkurugenzi wa halmashauri hiyo Katika maadhimiasho hayo yaliyofanyika katika Hospitali ya mji wa Njombe Kibena,Dokta Jabir amesema wapo baadhi ya wauguzi wamekuwa na tabia mbaya inayolalamikiwa na wagonjwa jambo ambalo halifai na atachukua hatua.
Baadhi ya wauguzi mkoani Njombe akiwemo Agnes Kihele na Gloria Mlowe wamekiri kuwapo kwa baadhi yao wanaoshindwa kuwakarimu wagonjwa na kuahidi kubadilika na kuiga mfano wa Muuguzi wa kwanza Night Ngale muasisi wa siku hiyo.
Aidha wauguzi hao wameiomba serikali kuendelea kushughulikia changamoto mbalimbali zinazowakabili katika kazi zao ili wafanye kazi vizuri ya kuwahudumia wagonjwa.
Kwa upande wao baadhi ya wananchi mjini Njombe akiwemo Agnetha Kihega na Paulina Lilauya wamesema hawajapata changamoto yoyote tangu wafike na kupata huduma katika Hospitali ya Kibena na kuwataka wauguzi wenye tabia mbaya kubadilika.
Naye Waziri Kindamba Imamu wa msikiti wa Kibena amesema kazi ya uuguzi inataka ukarimu mkubwa kwa wagonjwa na hivyo wanapaswa kufanyakazi hiyo kwa weledi mkubwa.
0 Comments