Header Ads Widget

TEMBO ALIYEUAWA MTU MOJA NA YEYE KAULIWA NACHINGWEA

Mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo amethibitisha kuuwawa kwa tembo mmoja na mwingine kujeruhiwa baada ya kuua mwananchi moja anayejulikana kwa jina la Fatma Chinguile katika kijiji cha Mwandila na kuharibu mazao ya wananchi katika wilaya hiyo.


Moyo alisema kuwa Tembo wamekuwa wakileta madhara makubwa kwa kuaribu mazao,makazi ya watu, kujeruhiwa na kuuwa watu hivyo serikali imeamua Tembo akiuwa au kujeruhiwa mtu basi na yeye auliwe hapo hapo.


Aidha Mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo ametaka wananchi kuchukua tahadhali pale wanapomuona au kukutana na Tembo ili kuokoa maisha yao.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI