Header Ads Widget

MBUNGE MAKANIKA ATOA LUNINGA KWA VIJIWE VYA KAHAWA

 


Na Fadhili Abdallah,Kigoma


Mbunge wa jimbo la Kigoma Kaskazini Asa Makanika ametoa msaada wa luninga nne kwa wananchi kwenye vijiwe vya kahawa katika vijiji vinne vya  halmashauri ya wilaya Kigoma jimbo la Kigoma Kaskazini ili kuwawezesha kupata taarifa mbalimbali za matukio ya kitaifa na kimataifa yanayoendelea duniani.


Makanika alikabidhi luninga nne ambazo kila Kijiji kilipata luninga moja ambazo zitatumika katika vijiiwe hivyo ambavyo vimekuwa na idadi kubwa ya watu hivyo kuwapa urahisi kupata Habari ambazo zitawafanya kujua mwenendo wa dunia.

 


Mbunge huyo alisema kuwa sambamba na Luninga hizo pia amekabidhi ving’amuzi ambavyo vitatumika Pamoja kwenye Luninga hizo ving’amuzi ambavyo vitawawezesha kuangalia mipira ya ndani ya nje ya nchi.


Akizungumza baada ya kukabidhiwa luninga hiyo Kiongozi wa kijiwe cha kahawa katika kijiji cha Nyarubanda, Twaha Seif alimshukuru mbunge kwa Luninga hiyo na kwamba itawasaidia kupata taarifa, matukio na kuangalia mipira ya ndani na nchi.


Luninga hizo zimetolewa pia kwenye vijiwe vya kahawa katika kijiji cha Matendo, Kumuhama na Pamila.


Mwisho

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI