Header Ads Widget

KITUO CHA MABASI SONGWE DC KUANZA MEI 15, DED AKUTANA NA WADAU

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Songwe CPA Cecilia Kavishe, amefanya kikao na wadau wa usafirishaji kujadili na kuweka mikakati ya namna ya kuanza matumizi ya Kituo kipya cha mabasi cha Wilaya ya Songwe (Kaloleni) ambacho kinatarajiwa kuanza kazi rasmi Jumatano ya Mei 15, 2024.


Kikao hicho kimefanyika Jumatatu (Mei 13, 2024) katika Ukumbi wa Sambila na kimehuduriwa na Mkuu wa Usalama Barabarani (DTO) Wilaya ya Songwe, wakuu wa Idara wa Halmashauri ya Wilaya ya Songwe, waheshimiwa madiwani wa Kata za Mkwajuni na Saza, wamiliki wa mabasi, viongozi wa wafanyabiashara, viongozi wa waendesha vyombo vya moto vikiwemo bodaboda na bajaji, watendaji wa kata za Mkwajuni na Saza pamoja na watendaji na wenyeviti wa vijiji vya kata za Mkwajuni na Saza.


Akizungumza katika kikao hicho, CPA Kavishe amesema kuwa tayari maandalizi yote yamekamilika kwa ajili ya stendi hiyo mpya iliyojengwa kwa mapato ya ndani ya Halmashauri kuanza kazi, ambapo baada ya kukamilisha ujenzi huo maandalizi ya awali yalifanyika ikiwa ni pamoja na kukamilisha vibanda vya baba/mama lishe, maeneo ya vibanda vya muda vya wafanyabiashara ndogondogo pamoja na maeneo maalumu ya waendesha bajani na pikipiki.



Aidha Mkurugenzi Mtendaji alitoa utaratibu wa vituo vingine vya kushushia na kupandia abiria kuwa ni Hospitali ya Wilaya, Ofisi za Halmashauri na Saza. Baadhi ya wadau waliomba kuwekwa kituo kingine katikati ya mji wa Mkwajuni.


Mkurugenzi Kavishe ameahidi kufanyia kazi mapendekezo yote pamoja na changamoto zitakazojitokeza wakati wa kuanza kutumika stendi hiyo mpya.


Pia aliwaomba wadau kuhamasisha na kusimamia mikakati na taratibu zilizoweka pamoja na kuwaelimisha wananchi kuwa tayari kuanza kutumia stendi mpya.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI