Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAAP NJOMBE
Madaktari bingwa 30 waliowasili mkoani Njombe hapo Mei 6 mwaka huu tayari wameanza kutoa huduma katika Hospitali za wilaya zote mkoani Hapa huku wito ukitolewa kwa wananchi kujitokeza kupata matibabu.
Mapema asubuhi kituo hiki kimezulu katika Hospitali ya mji wa Njombe Kibena na kushuhudia huduma zikiendelea kutolewa ambapo baadhi ya Wananchi waliopeleka wagonjwa akiwemo Grace Fungo wamekiri kukutana na Madaktari hao na kuanza kuwahudumia jambo linalosaidia kupunguza gharama za kwenda Rufaa katika mikoa mingine.
Erenestina Mwipopo Daktari Bingwa Mbobezi wa magonjwa ya Watoto anasema tayari ameanza kuwahudumia watoto na baadhi ya aliowahudumia ni wenye magonjwa ya Moyo,Kuzaliwa kabla ya wakati pamoja na Changamoto nyingine.
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mji wa Njombe Kibena Dokta Ayub Mtulo anasema ni fursa kwa wananchi wa Njombe kujitokeza katika Hospitali za Wilaya zinakopatikana huduma hizo kwani wataalamu hao wapo mkoani hapa kwa muda wa Siku tano pekee.
Magonjwa yanayohitaji huduma za Kibingwa yamekuwa na gharama kubwa jambo ambalo wananchi wa hali ya kawaida wamekuwa wakishindwa.
0 Comments